MVULANA WA MIAKA 11 AKIRI KUMBAKA MTOTO WA MIAKA SITA...

Mahakama ya Llandudno ambako kesi hiyo inasikilizwa.
Mvulana wa miaka 11 amekiri kumbaka msichana wa miaka sita jirani na nyumbani kwao mjini North Wales.
Mvulana huyo, ambaye hawezi kutajwa kwa sababu za kisheria, pia alikiri mashitaka matatu ya ubakaji kwa kumgusa na moja kati ya shambulio sugu kwa msichana huyo wa miaka sita pale alipofikishwa kwenye mahakama ya vijana ya Llandudno.
Wiki iliyopita mvulana huyo kutoka Gwynedd, mjini North Wales, alikana mashitaka pale alipofikishwa kwenye mahakama ya vijana ya Caernarfon.
Lakini juzi Jaji wa Wilaya Andrew Shaw alielezwa kwamba kumekuwapo majadiliano kati ya wazazi wa mvulana huyo, mwanasheria wake na daktari wake ambayo yalisababisha mabadiliko ya maelezo ya mshitakiwa mahakamani.
Wakili wa utetezi Nicola Jones alisema: "Baada ya majadiliano marefu mno na daktari wake, ambaye alimfahamu kwa miaka mingi, imefahamika wazi hakukuwa na chochote kitabibu ambacho kingeweza kumsababishia tabia ya aina hii.
Mvulana huyo alisindikizwa juzi wakati wa kusikilizwa kesi hiyo na baba yake na bibi yake. Baba yake alimkumbatia ubavuni dakika zote kumi za kusikilizwa kesi hiyo.
Jaji aliruhusu mvulana huyo aachiwe kwa dhamana yenye masharti hadi tarehe nyingine ya kusikilizwa kesi hiyo.

No comments: