Jordan (kushoto) akiwa na mama yake, Heidi. |
Mwanafunzi mvulana mwenye miaka 12 ambaye alienguliwa shuleni amejinyonga ikiwa ni masaa kadhaa tu baadaye, jopo la uchunguzi rasmi wa kisheria limeelezwa jana.
Jordan Green mwenye miaka 12, alitupa kwa nguvu viti kuzunguka chumba, kuapa mbele ya wafanyakazi na kuwatishia.
Mwanzoni alienguliwa shuleni hapo kwa siku moja na tabia yake ilipozidi kuwa mbaya kifungo hicho kikaongezwa hadi kufikia siku tano kabla baadaye mkuu wa shule hiyo kuamua kumfungia moja kwa moja.
Na alipomweleza mama yake, Heidi kuhusu kifungo hicho alisema: "Nakutakia maisha mema, najisikia kujiua mwenyewe".
Mama wa Jordan alisema alijaribu kumpigia baadaye, akaongeza: "Hakupokea simu yake na nilidhani 'kama kawaida yake kuwa hataki kuongea na mimi'."
Mtengeneza nywele huyo alisema alirejea nyumbani kwao huko Harrogate, North Yorkshire, baada ya Saa 2 usiku na kueleza: "Nilihisi kwamba hakuwapo nyumbani. Nilifikiri alikuwa akicheza na wenzake."
Madaktari wanaamini kwamba alikufa masaa kadhaa pale mwili wake ulipokutwa Juni 27 mwaka jana.
Jana, uchunguzi rasmi wa kisheria huko Knaresborough, mjini North Yorkshire, ulielezwa jinsi Jordan, ambaye mama yake alitengana na baba yake, Kevin, alivyokuwa mtukutu hata alipokuwa shule ya msingi.
Jordan alizidi kuwa mtukutu kwenye masomo tangu bibi yake alipofariki na wazazi wake kutengana, mama yake alilieleza jopo hilo.
Alipokwenda Harrogate High School, tania yake ikazidi kuwa mbaya, kumsababishia kuenguliwa kutoka kwenye masomo katika matukio kadhaa.
Mkuu wa shule msaidizi, Ann Francis alisema wafanyakazi walifanya mikutano kadhaa kuamua jinsi ya kumsaidia Jordan, ambaye alikuwa hodari kwenye masomo lakini mara kwa mara alitoroka darasani na kuwaapiza walimu.
Katika moja ya matukio hayo alianza kutimua mbio kuzunguka shule hiyo yenye wanafunzi 800 na kujificha asionekane na wafanyakazi wa shule hiyo ambao walikuwa wakimtafuta.
Lakini Juni uamuzi huo hatimaye ukafikiwa kumuengua kutoka shule hiyo kwa nia njema.
Asubuhi ya siku hiyo aliondoka nyumbani akiwa kachanganyikiwa baada ya kuwa amegoma kuinuka kitandani kwenda shule.
Alipofika hapo aliwekwa kwenye chumba kingine kumtuliza kabla ya kurejea kwenye masomo ya kawaida.
Ann alisema aliruhusiwa kutumia kompyuta katika chumba hicho na aliwekwa hapo sababu alionekana akisinzia.
Lakini takribani zaidi ya saa moja baadaye Jordan alitoka kwenye chumba hicho bila ruhusa na ndipo timu maalumu ya wafanyakazi ikaagizwa kwenda kumtafuta.
Ann alisema: "Alionekana kwenye sehemu tofauti za shule hiyo lakini hakuweza kusimama au kumsikiliza yeyoye."
Kwa karibu nusu saa, alikiri wafanyakazi hawakujua Jordan alikuwa wapi kabla ya kuonekana kwenye mgahawa lakini wafanyakazi walipojaribu kuongea naye aliwatukana na kutokomea kusikojulikana.
Hapo ndipo Mkuu wa Shule Andrew Bayston akaamua kumuengua Jordan kwa siku moja.
Lakini Jordan alipogundua wafanyakazi walikuwa wakijaribu kuwasiliana na wazazi wake akaanza kupiga mayowe 'mama anaumwa' na kuanza kurusha vitu hovyo, vikiwamo viti.
Ann alisema: "alikuwa akilalama na kupiga kelele akitukana wafanyakazi ambao waliamua kumwacha kwenye chumba ili kumtuliza."
Wakati fulani wanafunzi wa darasa lingine walilamika kuhamishiwa chumba kingine sababu walikuwa wakiona kilichokuwa kikiendelea.
Na kufuatia tabia ya Jordan mkuu wa shule akaongeza kifungo hicho kufikia siku tano.
Muda mfupi baada ya kuondoka shuleni, Jordan akarejea kuchukua pikipiki yake na dakika kadhaa baadaye akarejea, akiulizia chakula na akapatiwa kiasi.
Lakini baada ya mkutano kati ya wafanyakazi, mkuu wa shule akaamua kwamba Jordan afukuzwe shuleni hapo moja kwa moja.
Baada ya uamuzi huo kufanywa, ikabakia juu ya mamlaka kuamua kuhusu hatima ya baadaye ya Jordan.
Ann alisema taarifa kwamba Jordan, ambaye alikuwa akiishi na mama yake, amekuwa akiteswa hayakuwa sahihi na Jordan hakuwahi kuripoti kwamba amekuwa akiteswa.

No comments:
Post a Comment