Viongozi wa makanisa makubwa ya kiprotestanti nchini, wametajwa kutumia imani ya jumuiya ya kimataifa kwao, kuibia wahisani mabilioni ya fedha za miradi ya kusaidia watu wasiojiweza wakiwamo yatima.
Taarifa za uhakika kutoka shirika la wahisani la Marekani zilizotufikia, zimebainisha kuwa wizi na ubadhirifu umekuwa ukifanywa na viongozi hao wakiwamo maaskofu kwenye fedha za misaada.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mashirika hayo yaliamua kutumia makanisa baada ya kupoteza imani na serikali za kiafrika, ambazo zinatuhumiwa kufuja fedha za misaada.
Kutokana na imani yao kwa makanisa ambayo yameelezwa kutokuwa na uhusiano na serikali hizo, taarifa ya wahisani hao imeeleza kuwa kabla ya kutoa misaada, huingia makubaliano kuhusu jamii inayopaswa kunufaika na msaada husika.
Viongozi hao wa makanisa wanadaiwa kuwa wakati wa kuingia makubaliano, husisitiza mfumo wa ushirikiano uzingatie mradi unaosaidiwa kuwa chini ya Kanisa, utekelezaji wake usiingiliwe na wahisani wa nje na uwekezaji uzingatie vipaumbele vya Kanisa husika na si wahisani.
“Kinadharia, inaonekana ni suala jema na la maendeleo. Lakini katika utendaji, vikwazo vinaanza kwa viongozi wa Kanisa kukwepa uwajibikaji katika miradi kwa kisingizio cha kutoingiliwa na wahisani.
“Wahisani wakiomba ripoti za ukaguzi wa miradi na wa matumizi ya fedha ili kulinganisha kama miradi ina thamani ya fedha husika, hukabiliwa na tuhuma kwamba wanaleta ukoloni na ubaguzi wa rangi,” ilieleza taarifa hiyo.
Kutokana na tuhuma hizo, taarifa hiyo ilieleza kuwa wahisani hao hasa wanaotoa misaada kupitia Kanisa, hujikuta wakilazimika kuacha kudai taarifa zozote kuhusu miradi hiyo.
“Wakati wa utekelezaji wa miradi ya afya na elimu, maaskofu wa makanisa hayo hudaiwa kushirikiana na maofisa wa Uhamiaji, kuhakikisha wawakilishi wa wahisani hao wananyimwa kibali cha kuishi nchini na kufukuzwa nchini.
Baada ya kufukuza wawakilishi wa wahisani hao nchini, maaskofu hao wanadaiwa kuiba mali za miradi na nyingine hutumika kujenga nyumba binafsi za maaskofu.
“Tangu uhuru serikali za Afrika zimekabiliwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma na mfano wa kihistoria ni Serikali ya Uganda chini ya Dikteta Iddi Amini na ya Kongo chini ya Mobutu SeseSeko.
“Kutokana na mwonekano huo, ilionekana njia nzuri zaidi ya kutoa misaada Afrika ni kutumia taasisi za imani kwa kuwa zinafanya kazi kwa uhuru bila kuingiliwa na Serikali…kwa bahati mbaya viongozi wa dini wamegeuka sura mpya ya rushwa Afrika,” imeeleza taarifa hiyo.
Wahisani hao wamedai kuwa lengo la kutoa taarifa hiyo si kuinyima Afrika misaada kwa kuwa Waafrika bado wanahitaji misaada, lakini wanalazimika kuwa na mikakati mipya ikiwamo kuongeza masharti ili kuhakikisha fedha zinafikia walengwa.

No comments:
Post a Comment