PAPA WA TANI 33 AVUNJA TANGI NA KUJERUHI 15...

Wafanyakazi wakikusanya mabaki ya vioo mara baada ya ajali hiyo.
Hili ni tukio ya kushitusha pale papa mwenye tani 33 alipovunja uzio wa tangisamaki na kujeruhi watu 15 kutokana na kukatwa na vipande vya vioo vilivyorushwa angani na maji yaliyobubujika kwa kasi kubwa.
Tangi hilo lilikuwa kivutio kwenye lango la kuingilia eneo lenye maduka mengi la Shanghai Orient katika jiji la pili kwa ukubwa nchini China pale ilipofungwa bila notisi Desemba 19.
Watu nane kati ya wote waliojeruhiwa walikuwa wateja na wengine walikuwa wauzaji kwenye maduka na walinzi. Wengi wao walipata majeraha ya kukatwa vibaya na kukwaruzwa kwa vipande vya vioo vilivyovunjika.
Msemaji wa polisi alisema: "Kulikuwa na majeruhi wengi waliosababishwa na kukatwa vipande vya vioo vilivyorushwa, baadhi yao hali zao zikiwa mbaya sababu kioo kilikuwa kipana mno. Tunachunguza kujua nini hasa kilichosababisha tukio hili."
Papa watatu wa rangi ya limao na makumi ya kasa na samaki wadogo, ambao walikuwa wakihifadhiwa kwenye tangisamaki hilo, walikuwa ni miongoni mwa waathirika wa ajali hiyo ambayo ilinaswa kwenye kamera za CCTV.
Wateja walikimbia kwa kiwewe wakati kioo cha upana wa sentimeta 15 kilipokuwa kikianguka, kuvurumisha maji kwenye lango la kuingilia katika jengo hilo la maduka mengi.
Wakati hakuna sababu rasmi iliyotolewa kuhusu ajali hiyo, wateja walisema kwamba wanaamini kushuka ghafla kwa joto kunaweza kuwa sababu ya kupasuka, huku hali ya hewa jijini Shanghai ikiendelea kuwa ya baridi wiki iliyopita.
Tangisamaki hilo limeripotiwa kuwa maarufu sana pale lilipozinduliwa kwa mara ya kwanza kabla ya mapumziko ya Sherehe za Siku ya Taifa hilo miaka miwili iliyopita, lakini kumekuwa na matatizo na tangi hilo kabla, pale Juni bomba la maji lililopasuka liliposababisha vifo vya papa wawili na kasa kadhaa kuondolewa.
Ofisa katika uongozi wa eneo hilo lenye maduka mengi, Chen Yongping, alisema kwamba hawafikirii 'kujenga tena tangisamaki katika siku zijazo'.

No comments: