POLISI WAKAMATA KILO 1,640 ZA BANGI INAYOPELEKWA UINGEREZA...

Waingereza wawili ni miongoni mwa watu 51 waliokamatwa wakati polisi walipovunja kundi kubwa la kimataifa la usafirishaji dawa za kulevya na kuifanya Uingereza kufurika kwa mihadarati.
Polisi wa Hispania wamekamata kilo 1,640 za bangi zenye thamani ya Pauni za Uingereza milioni 5 pamoja na boti nne ziendazo kasi, magari 17, malori na pikipiki zinazotumika kusambazia dawa hizo.
Polisi walisema mtandao huo unaundwa na Wahispania, Wamorocco, Warusi, Waingereza, Wajerumani, Waholanzi na Waromania.
Wanatuhumiwa kufanya magendo ya bandi zenye thamani ya mamilioni ya Pauni kutoka Afrika kwenda Ulaya.
Maofisa wenye silaha wamepekua vifaa 11 na kompyuta zilizokamatwa, simu za mikononi na mashine zinazotumika kufungia dawa hizo.
Waingereza hao wawili walikamatwa mjini Coin karibu na Malaga.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Hispania imesema kwenye taarifa yake kwamba: "Mtandao huu ulisafirisha dawa hizo kwa kutumia boti ziendazo kasi kutoka Morocco, na kupakua kwenye fukwe mbalimbali katika pwani ya Hispania kisha baadaye kuzificha ndani ya magari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nchi nyingine za Ulaya.
"Dawa hizo zilizokuwa zikielekea Uingereza zilifungwa kwenye ghala huko Coin, Malaga, ambako polisi waligundua chumba cha siri, kilichofichwa nyuma ya makabati, wakitumia mgandamizo wa hewa kwenye utomvu wa bangi hiyo."
Dawa hizo za kulevya zilikamatwa katika vitongoji vya Malaga, Seville, Alicante, Girona, Barcelona na Cadiz.
Polisi hawakutoa taarifa zozote zaidi kuhusu Waingereza hao wawili walio chini ya ulinzi.

No comments: