CHEKA TARATIBU...

Mhudumu wa ndege kamfuata Mzee wa Kisukuma na kumtaka kuhama sehemu alipokaa katika daraja la kwanza na kwenda daraja la kawaida anakostahili. Mzee wa Kisukuma akagoma akijitetea yeye ni maarufu na kwamba hatoki pale mpaka afike Mwanza. Baada ya karibu nusu saa ya mabishano bila mafanikio, Mhudumu akamwita Bosi wake amsaidie kuongea na yule mzee. Bosi akamfuata yule mzee na kumnong'oneza. Haraka sana yule mzee akainuka na kwenda kukaa sehemu anapotakiwa. Kwa mshangao Mhudumu akamuuliza Bosi wake katumia mbinu gani kumhamisha yule mzee kirahisi vile. Bosi akajibu, "Nimemweleza tu kwamba sehemu aliyokaa haiendi Mwanza!" Kasheshe...

No comments: