MAMA AMUUA MWANAE KWA KUSHINDWA KUHIFADHI AYA ZA QUR'AN...

KUSHOTO: Yaseen Ali enzi za uhai wake. KULIA: Mwili wa Yaseen ukipelekwa kuzikwa.
Mama amempiga vibaya kwa fimbo hadi kufa mtoto wake wa kiume mwenye miaka saba kisha kuchoma moto mwili wake sababu alikuwa mzito kushika kichwani aya za Qur'an Tukufu, mahakama ilielezwa.
Sara Ege mwenye miaka 32, anadaiwa kumpiga mtoto wake Yaseen Ali 'kama mbwa' kwa kushindwa kuelewa aya kutoka kwenye maandiko hayo matakatifu, kabla ya kuuchoma moto mwili wake katika nyumba yao iliyoko mjini Cardiff katika harakati za kuficha uovu wake huo alioufanya.
Kifo cha kijana huyo kinaaminika kuwa janga kufuatia moto kwenye nyumba huko Pontcanna, hadi hapo uchunguzi wa mwili ulipogundua Yaseen alikufa kabla ya moto kulipuka, Mahakama ya Cardiff imeelezwa.
Sara pia anatuhumiwa kwa kumtesa mtoto wake huyo wa kiume kwa miezi kadhaa kuelekea kifo chake, akidaiwa kumpiga kwa nyundo na kumfungia bandani kwa kuwa mzito katika kuelewa masomo ya Kiislamu.
Kesi hiyo katika Mahakama ya Cardiff imeelezwa jinsi mhitimu huyo wa Chuo Kikuu na mumewe, Yousuf Ege walimwingiza Yaseen katika madarasa ya juu kwenye msikiti wa jirani na kutarajia angekuja kuwa Hafiz - neno la Kiislamu linalotumiwa kwa mtu ambaye ameshika vilivyo aya za Qur'an kichwani.
Katika video iliyorekodiwa ya mahojiano na polisi, Sara aliwaeleza maofisa alimwekea malengo mtoto wake huyo wa miaka saba kuweza kushika kurasa 35 katika miezi mitatu.
Lakini mahakama ilielezwa Yaseen mwenye kupenda ucheshi alipendelea kucheza na marafiki zake na kuzorota kwenye masomo yake.
"Nilizidi kuchanganyikiwa zaidi na zaidi," Sara alisema katika mahojiano hayo.
"Kama akishindwa kusoma vizuri nilipanda  mno na jazba - Nilimpiga.
"Lakini Yaseen hakuwa mahiri - baada ya mwaka wa mafunzo aliweza kushika sura moja tu."
Aliendelea: "Nilijawa na uchafu wote huu kichwani mwangu, kama sikuweza kuzingatia, nilipandwa na hasira mno, nilimgombeza Yaseen wakati wote.
"Nilizidi kupata wazimu - Nilitumia fimbo kumtandika nayo."
Mahakama ilielezwa jinzi Sara alivyompiga Yaseen kwa nyundo, na kandambili na pia kumshindilia ngumi mfululizo.
Pia anatuhumiwa kumfungia katika banda, kumfunga kwenye mlango, na kumlazimisha kufanya kushapu.
Mahakama ilielezwa kwamba miezi kadhaa baada ya kifo cha Yaseen, Sara alimweleza daktari alielekezwa na Shetani kumuua mtoto wake huyo wa kiume - na kwamba alikuwa akijisikia vizuri kwa asilimia mia moja baada ya kifo chake.
Maelezo aliyojirekodi yaliyopatikana yanasema: "Ni kama kuna kitu kimeachilia. Kwa miezi mitatu au minne sikuwa katika hali ya kawaida."
Polisi na vikosi vya uokoaji viliitwa kwenye nyumba hiyo huko Pontcanna, mjini Cardiff, Julai 2010 baada ya moto kuchomoza katika ghorofa ya juu.
Yaseen alivutwa kutoka kwenye moto na askari wa uokoaji Rhodri Morgan aliieleza mahakama jinsi alivyomhudumia akiamini pengine anaweza kuokoa maisha yake.
Alisema: "Nilikuwa nikimkandamiza kifua chake kurejesha mapigo ya moyo, lakini nililazimika kutoa mikono yangu sababu ngozi yake ilikuwa ya moto sana.
"Nilipokuwa nikifanya hivyo vipande vya ngozi yake na mafuta yalikuwa yakichuruzika kutoka miguuni mwake - ilikuwa kama kipande cha karatasi kilichoungua na kukunjamana."
Mafuta ya kuchomea nyama walikutwa katika nguo za Sara wakati alipokamatwa baada ya uchunguzi wa mwili kugundua kwamba Yaseen alikufa kabla ya moto kulipuka.
Alikana kumuua Yaseen na kuuchoma mwili wake kufika kile alichokuwa amefanya.
Mumewe  anakanusha kusababisha au kuruhusu kifo cha mtoto huyo kwa kutozuia vipigo hivyo vya mkewe.
Baba wa Yaseen, ambaye alimpelekea mtoto huyo wa miaka saba kwenye msikiti kwa ajili ya mafunzo ya Qur'an kabla na baada ya kuanza shule, amesema hakuwahi kumuona mkewe akiinua mkono kumpiga mtoto wao. Kesi hiyo inaendelea.

No comments: