KABURI LA BINTI MFALME LA TANGU MWAKA 1930 LAVUMBULIWA MISRI...

Kaburi wa Binti Mfalme la tangu mwaka 2500 BC (Kabla ya Kristo) limevumbuliwa karibu na Cairo, Serikali ya Misri imebainisha jana.
Uvumbuzi huo umefanyika katika mji wa Abu Sir kusini mwa Cairo na timu ya wanaakiolojia kutoka Czechoslovakia.
"Tumevumbua chumba cha kusubiria kuelekea kwenye kaburi la Binti Mfalme Shert Nebti ambalo linajumuisha mihimili ya mawe ya chokaa," alisema Mohamed Ibrahim, Waziri wa mambo ya kale wa Misri.
Mihimili hiyo 'ina maandiko ya hieroglifu yakitambulisha jina la Binti Mfalme na anwani zake, ikijumuisha 'binti wa Mfalme Men Salbo na mpenzi wake alitukuzwa mbele ya Mungu kuwa mwenye nguvu zaidi," aliongeza.
Ibrahim alisema kwamba Taasisi ya Czech inayotafiti Mambo ya Kale ya Misri, inayofadhiliwa na Chuo Kikuu cha Charles cha Prague na kuongozwa na Miroslav Bartas, ndiyo iliyofanikisha uvumbuzi huo.
"Kuvumbuliwa kwa kaburi hili kumeweka alama ya mwanzo wa zama mpya katika historia ya makaburi katika Abu Sir na Saqqara," alisema Ibrahim.
Timu hiyo ya Czech pia imechimbua mlango wa nyuma huko kusini mashariki mwa chumba cha kusubiria, ambacho kinaelekea kwenye makaburi mengine manne, mawili kati ya hayo tayari yameshavumbuliwa wakati tofauti.
Makaburi mawili ni ya maofisa wa ngazi za juu wakiwamo 'mtetea sheria mkongwe' na 'mkaguzi wa wahudumu wa jumba la mfalme,' kwa mujibu wa maandiko. Yamewekwa tarehe kuanzia utawala wa tano wa kifirauni.
Uvumbuzi huo umefanyika wakati wa msimu wa uchimbuaji, ambao umeanza Oktoba, alisema Usama al-Shini, Mkurugenzi wa Baraza Kuu la Mambo ya Kale huko Giza.
Kibaraza hicho kinajumuisha majeneza manne ya mawe ya chokaa ambayo yana sanamu ya mtu, mwanaume akiwa na mtoto wake wa kiume, na wanaume wawili wakiwa na mwanamke.

No comments: