CHEKA TARATIBU...

Katika mwanzo wa miaka ya 1930, mkulima mmoja na mkewe walikwenda kwenye maonesho. Mkulima alivutiwa mno na maonesho ya ndege na kumuuliza rubani inagharimu kiasi gani kkwa safari moja. Rubani akajibu, "Shilingi Laki Moja kwa dakika tatu." Mkulima akajibu kwa mshangao, "Duh, gharama kubwa sana!" Rubani akafikiria kwa sekunde chache kisha akasema, "Endapo wewe na mkeo nitawazungusha hewani kwa dakika tatu bila kupiga kelele sitawatoza chochote. Lakini mkipiga kelele itabidi mlipe Shilingi Laki Moja." Mkulima na mkewe wakakubali na safari ikaanza. Baada ya ndege kutua, Rubani akamweleza Mkulima, "Napenda kukupongeza kwa kutopiga kelele. Wewe ni mwanaume jasiri." Mkulima akajibu, "Inawezekana," Lakini napenda kukwambia ilibaki kidogo tu nipige kelele wakati mke wangu alipoanguka angani kutoka kwenye ndege!" Duh…

No comments: