Wanawake wawili wa Uingereza wamestahimili masaa manne ya kutisha wakiwa wamenasa chini ya boti ya kitalii baada ya kupinduka kwenye maji yaliyojaa papa karibu na Cape Town.
Lynette Hartman mwenye miaka 55, na Bronwyn Armstrong walinasa chini ya moja ya maganda mawili na wakisaidiwa na mifuko ya kupumulia ya hewa.
Watalii mwenzao Peter Hyett mwenye miaka 64 wa Vale of Glamorgan, huko Wales ya kusini, alikufa baada ya boti ndogo, ambayo ilikuwa imebeba watu 40 kupinduka majira ya Saa 8 mchana Jumamosi.
Wanawake hao wawili wa Uingereza walikutwa wakiwa wamening'inia pembeni ya boti hiyo wakati wazamiaji wakitafuta miili na waokoaji waliwasiliana kwa kunasa maganda hayo.
Huku joto la bahari likiwa chini ya nyuzijoto 10, isingekuwa rahisi kwao kuweza kuendelea kuwa hai kwa muda wa saa moja zaidi kama wangekuwa kwenye maji ya wazi.
Wazamiaji wa polisi waliwapatia vifaa vya kuwasaidia kupumua kabla ya kuwashawishi wavue majaketi yao ya kujiokolea hivyo kuweza kuogelea na kujinasua kwenye kina cha futi 36.
Craig Lambinon, kutoka Taasisi ya Taifa ya Bahari na Ukoaji, alisema abiria karibu wote waliokolewa kwa kutumia boti ndogo zilizokuwa maeneo ya jirani.
Lakini alisema wanawake hao wawili 'walikuwa wamenaswa wakati boti yao ilipopinduka na kupata mfuko wa hewa uliowasaidia kuweza kupumua', alisema Craig.
"Walikuwa wameganda kwa ubaridi huku wakiwa wamevalia majaketi yao ya kujiokolea na nguo zao za kawaida tu.
"Waokoaji walifanikiwa kuwakuta lakini walikuwa wamejawa hofu mno na ilichukua muda mrefu kuweza kuwashawishi wavue majaketi yao na kuogelea kutoka eneo hilo.
"Wanawake hao walilazimika kupewa mafunzo ya kutumia vifaa vya kusaidia kupumua na hatimaye waliweza kuokolewa majira ya Saa 11:50 jioni."
Hyett aliopolewa na kupelekwa ufukweni, ambako ilitangazwa baadaye kwamba amefariki dunia.
Mke wa Mwingereza huyo aliyekufa Suzanne, mwenye miaka 63 na binti yake Helen mwenye miaka 37 wakazi wa Bournemouth, walinusurika katika ajali hiyo na walikuwa wakiendelea na matibabu hospitalini.

No comments:
Post a Comment