RICK ROSS ADUNDANA NA JEEZY NYUMA YA JUKWAA...

Rick Ross (kushoto) na Young Jeezy.
Imefahamika kwamba zilipigwa ngumi kavukavu nyuma ya jukwaa wakati wa Tuzo za BET za Hip Hop juzi kati ya Rick Ross na Young Jeezy zilizopelekea kutupishiana risasi kwa mujibu wa vyanzo vya habari.
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, Ross na Jeezy walitupishiana maneno na kuanza kusukumana na kisha kubimbirishana. Imeelezwa walinzi wa BET na mabaunsa wa kila rapa waliingilia kati na kufanikiwa kuwatenganisha wawili hao.
Vyanzo kutoka eneo la tukio vilisema kwamba baada ya mapigano hayo kuzimwa, mfuasi wa kundi la Rick Ross alitoa bunduki wakati akiwa kwenye eneo la maegesho ya magari na kufyatua risasi kadhaa.
Imeelezwa kuwa Jeezy na Ross bado wamo katika kinyang'anyiro cha tuzo hizo, ambazo zimerekodiwa siku hiyo mjini Atlanta na kurushwa hewani mwezi ujao.
Rick Ross anatarajiwa kutua Dar kwa ajili ya kufanya shoo kwenye Tamasha la Fiesta 'Bhaaaaaas' mwishoni mwa wiki hii, ambalo huandaliwa na Clouds Media Group kila mwaka.

No comments: