Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. |
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imekamata meno ya tembo yenye thamani ya Sh bilioni 2.1, yakiwa katika viroba vilivyofunikwa na Bendera ya Taifa, na kuhifadhiwa katika nyumba eneo la Kimara Stop Over, Kinondoni.
Akizungumza ofisini kwake jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema baada ya kukamata nyara hizo za Serikali juzi saa 6.30 mchana, wataalamu wa Maliasili walifanya majumuisho na kubaini kuwa yalitokana na tembo 91 waliouawa.
Mbali na nyara hizo, pia walikamata watuhumiwa wanne wa uhalifu huo, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa raia wema.
Nyara hizo na mali zingine zinazodaiwa kuibwa na majambazi katika matukio mbalimbali Dar es Salaam, kwa mujibu wa Kova, zilikutwa ndani ya nyumba ya Peter Kami, raia wa Kenya anayeishi na mwanamke Mtanzania, Leonida Kabi.
Wengine waliokamatwa ndani ya nyumba hiyo ni Charles Wainaine (41) ambaye ni ndugu wa Leonida na dereva wa daladala, Polisi Simon (42).
“Tunawashukuru raia wema wanaoendelea kushirikiana nasi kupambana na uhalifu na tunawaomba waendelee hivyo hivyo, maana hata kukamata watu hawa, ndio wamefanikisha,” alisema Kova.
Idadi ya meno hayo ni 214 na yaliyokuwa katika viroba 12. Sambamba na men ohayo pia kulikutwa pembe 10 za ng’ombe zikiwa zimeshindiliwa chokaa na mifupa mitano ya tembo.
Alifafanua kuwa katika kubaini idadi ya tembo waliouawa, wataalamu wa Maliasili walifanya majumuisho ya kitaalamu ya meno na mifupa hiyo na kugundua kuwa na jumla ya kilo 450.6 ambazo ni sawa na tembo 91.
Kwa mujibu wa Kova, uchunguzi wa awali ulionesha kuwa watu hao ni wahalifu wazoefu katika matukio mbalimbali ya kijambazi pamoja na usafirishaji na umiliki wa nyara za Serikali.
Pia alidai kwamba walikuwa na mpango wa siri wa kusafirisha meno hayo kwa kutumia gari aina ya Toyota Coaster linaloendeshwa na Simon.
“Kulikuwa na mpango wa siri wa kusafirisha meno haya kwa kutumia Coaster (Toyota) ambapo wangeweka jeneza lililofunikwa Bendera ya Taifa kama vile wanasafirisha maiti ya mtu maarufu serikalini.
“Lengo lilikuwa kuhadaa vyombo vya Dola na Mamlaka husika; nyara hizi zingevushwa kwenda nje kupitia mpaka wa Tarakea, Rombo kwenda Kenya,” alisema Kova.
Alisema Leonida anashikiliwa kwa tuhuma zingine za kushawishi askari waliokamata mali hizo kupokea rushwa ya Sh milioni 15 kama kianzio na kuwaahidi nyingine siku inayofuata, baada ya benki kufunguliwa, ambapo askari hao walikataa na kuwapeleka kituoni.
Kova alisema uchunguzi unaendelea kufanyika ili kubaini mtandao wa wizi wa nyara za Serikali nchini na nje ya nchi na watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
“Hawa askari walishawishiwa kupokea rushwa lakini walikataa, nawapongeza sana na kuna zawadi ambazo nitawapa, kwa sababu wameonesha ujasiri wa hali ya juu na kutanguliza utaifa,” aliongeza Kova.
Katika tukio lingine, Polisi wakishirikiana na ulinzi shirikishi wamemkamata Swalish Rweyemamu (23) kwa tuhuma za wizi wa pikipiki na mali mbalimbali akiwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Alisema mtuhumiwa huyo anadaiwa kujifanya abiria na kukodi pikipiki na baada ya kufika mbele, alimnyang’anya dereva wa pikipiki ya bodaboda baada ya kumtishia bastola bandia.
Kamanda Kova alisema walipomkamata mtuhumiwa na kumpekua, walikuta kitambulisho kilichotolewa na JWTZ cha namba (TPDF) DFF 7001 831 KJ na anuani S.L.P. 1992 Dar es Salaam.
Kitambulisho hicho kwa mujibu wa Kova kilitolewa Machi 13, 2008 kwa jina la MT. 84187 Ahmed Salum. Pia alikutwa na nguo za kiraia ambazo inadaiwa hubadilisha baada ya tukio.

No comments:
Post a Comment