MWANAMKE ABAKWA MARA MBILI KATIKA MATUKIO TOFAUTI USIKU MMOJA...

KUSHOTO: Mtuhumiwa wa kwanza wa ubakaji, Yussuf. KULIA: Eneo ambapo tukio hilo la ubakaji lilifanyika.
Mwanamke ambaye alikokotwa kwenye kichochoro na kubakwa akitoka matembezini usiku alikumbana na tukio lingine la kutisha kwa kubakwa na mwanaume mwingine wakati akijizoazoa baada ya shambulio la kwanza.
Mustafa Yussuf ndiye alikuwa wa kwanza kumbaka mwanamke huyo wakati akitembea katikati ya jiji la Manchester katika Sherehe za Mwaka Mpya, akipita kwenye maegesho ya magari yaliyoko Church Street na kumbaka karibu kabisa na barabara.
Baada ya shambulio hilo mwanaume huyo aliyekuwa na miaka 20 wakati huo akitoweka eneo la tukio, akimwacha mwanamke huyo bila msaada wowote.
Ni wakati huo ndipo, badala ya kumsaidia, mwanaume mwingine akamvamia mwanamke huyo na kuanza kumbaka tena.
Habari za matukio hayo mawili ya ubakaji zimebainika wakati Yussuf ambaye sasa ana miaka 21, mkazi wa Manchester, akihukumiwa kifungo cha miaka saba jela kutokana na shambulio hilo.
Alidai kufanya mapenzi na mwanamke huyo lakini akakanusha kumbaka.
Lakini Baraza katika Mahakama ya Manchester limetupilia mbali utetezi wake na kumtia hatiani.
Jaji Martin Steige, akitoa hukumu, alisema hana shaka kwamba Yussuf alifahamu kabisa kwamba mwanamke huyo alikuwa amelewa mno kiasi cha kutojitambua.
Mahakama ilielezwa kwamba mwanamke huyo 'mtu mzima' alikunywa kupita kiasi sababu ya matatizo yake ya kimapenzi, huku kamera za CCTV zikimuonesha akiwa hawezi kusimama.
Alizuiwa kuingia tena kwenye klabu ya usiku wakati alipotaka aruhusiwe kuingia akatafute begi lake dogo la mkononi alilopoteza ndani ya klabu hiyo.
Baada ya kubakwa mara mbili, mwanamke huyo alihitaji msaada kutoka kwa watu baki kuweza kufika nyumbani kwake na kwa masaa mawili hakuweza kabisa kukumbuka kilichomtokea.
Muathirika aliieleza mahakama kwamba maisha yake yamezimwa kufuatia shambulio hilo na ametengwa kwa hofu ya kutembea nje.
Jaji Steiger alisema: "Wakati fulani baada ya shambulio la kwanza alibakwa tena na mtu mwingine."
Mwanaume mwingine alikamatwa kufuatia shambulio la pili la ubakaji lakini akaachiwa bila kufunguliwa mashitaka yoyote.

No comments: