MTOTO ALIYEBAKWA NA KUCHOMWA MOTO AFARIKI DUNIA...


JUU na CHINI: Robbie Middleton kabla ya shambulio. KATIKATI: Robbie Middleton akiwa kitandani muda mfupi kabla ya kifo chake. KULIA: Mtuhumiwa Don Collins.
Katika siku yake ya kumbukumbu ya miaka minane tangu kuzaliwa kwake alikuwa amefungwa kamba katika mti, akamwagiwa petroli na kuchomwa moto.
Tukio hilo la kikatili limemwacha Robbie Middleton katika kiwango cha juu kabisa cha kuungua kwa asilimia 99 ya mwili wake. Hakuna aliyetarajia kama angepona.
Lakini katika historia ya hamasa ya ajabu, Robbie akaendelea kuishi. Alilazimika kufanyiwa oparesheni 200 na matibabu yasiyo na ukomo kukarabati majeraha yake ya moto.
Kwa huzuni, akafariki dunia wiki chache kabla ya kutimiza miaka 21 kutokana na saratani ambayo madaktari wamelaumiwa kwamba ilitokana na majeraha yake ya mwanzo.
Kwenye video ya dakika 17 iliyotengenezwa muda mfupi kabla hajafa, alimtaja mtu ambaye anaamini alimuwasha moto huko Splendora, mjini Texas mwaka 1998.
Na pia akadai kwamba alibakwa na mtu huyo huyo, jirani yake mwenye miaka 13 anayefahamika kwa jina la Don Collins, wiki mbili kabla ya kuchomwa moto.
Madai yake hayo yamefungua njia kwa Collins, ambaye sasa ana miaka 27, kufunguliwa mashitaka ya ubakaji, kushitakiwa kwa jinai ya mauaji.
Robert Ray 'Robbie' Middleton alikuwa akisherehekea kutimiza miaka minane Aprili 29, 1998 ndipo alipokutana na jirani yake Don Collins kwenye mlango wa mbao karibu na nyumba yao huko Splendora, Montgomery County.
Wiki mbili kabla, kwa mujibu wa taarifa ya Robbie Middleton kabla ya kifo chake, wawili hao walikutana sehemu hiyo na Collins ambaye wakati huyo alikuwa na miaka 13, akamzidi nguvu kijana huyo mdogo na kumbaka. Sasa anataka anyamazishwe.
"Don alinishika kwa nguvu mabegani na kunipulizia gesi usoni, baada ya hapo sikumbuki kilichoendelea," Robbie Middleton alisema kupitia taarifa yake ya video.
Mwaka 2001, akiwa na miaka 16, Don Collins alihukumiwa kifungo kwa shambulio la kubaka mtoto wa miaka minane.
Mama wa Robbie, Colleen na mumewe Bobby walishinda kesi dhidi ya Don Collins mwaka 2001, na kulipwa Dola za Marekani bilioni 150, kiwango kikubwa cha fidia kuwahi kutolewa katika historia ya Marekani.
Si Collins wala mwanasheria wake yoyote aliyejitokeza kumwakilisha katika usikilizwaji wa kesi hiyo.

No comments: