MFANYABIASHARA SALIM ABRI ASAS ACHANGIA UJENZI WA MABWENI KILOLO...

Mfanyabiashara Salim Abri (kulia) katika picha ya pamoja na viongozi mara baada ya kukabidhi mifuko hiyo ya saruji.

Salim Abri (wa pili kulia) akikabidhi mifuko 200 ya saruji kusaidia ujenzi wa mabweni wilayani Kilolo.
Mfanyabiashara maarufu, Salim Abri Asas ametoa msaada wa mifuko ya saruji 200 yenye thamani ya  zaidi ya Shilingi milioni 3.2  ikiwa ni mchango wake katika ujenzi  wa mabweni ya wasichana katika  shule  nne za Sekondari  zilizoko katika Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Akikabidhi  msaada  huo ofisini kwake,  Asas ambaye pia ni Kamanda  wa Umoja  wa Vijana  wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa  wa Iringa, alisema  kuwa amelazimika  kuchangia  ujenzi huo wa mabweni ikiwa ni  sehemu ya  kuiunga mkono serikali  iliyopo madarakani  chini ya Rais Jakaya  Kikwete katika kuinua kiwango cha elimu ambapo elimu imekuwa ikipewa kipaumbele  zaidi.
Alisema  kuwa mbali ya  kuchangia ujenzi huo katika  wilaya ya  Kilolo pia ameshafanya hivyo katika Halmashauri ya  Manispaa ya Iringa na maeneo mengine  ya mkoa wa Iringa.
Alisema  kuwa wilaya ya Kilolo kupitia kwa Mkuu wa Wilaya waliandika barua kwake  kuomba kusaidiwa ujenzi wa  Shule za Sekondari na mabweni katika  wilaya  hiyo ya  Kilolo.
Kwa  upande  wake  Mkuu  wa  Wilaya ya  Kilolo, Gerald Guninita  mbali ya  kumpongeza Asas ambaye pia ni mmoja kati ya  wafanyabiashara  wakubwa mkoani Iringa,  aliwaomba  wadau zaidi wa elimu  katika  mkoa  wa Iringa wakiwemo  wafanyabiashara  kujitokeza  kuchangia  maendeleo ya  elimu katika  wilaya hiyo ya Kilolo.
Hata  hivyo  mkuu  huyo wa wilaya  alisema  kuwa saruji  hiyo   itagawanywa mifuko 50 kwa shule  nne  za  sekondari ambazo zinaendelea na ujenzi  wa mabweni ya  wanafunzi wa  kike.
Alizitaja  shule za  sekondari ambazo zitanufaika na msaada huo  kuwa ni Uhambingeto, Gangwa, Ukwega na Masisiwe.

No comments: