Shekhe Farid Hadi Ahmed. |
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa amesema Polisi inafanya uchunguzi wa kina kubaini kama kiongozi wa Uamsho, Shekhe Farid Hadi Ahmed anahusika na mtandao hatari wa ugaidi wa Al-Qaeda.
Akizungumza jana, Mussa alisema Polisi nchini inafanya kazi hiyo kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa ikiwamo Polisi - Interpol.
“Jeshi la Polisi nchini kwa sasa linafuatilia kwa karibu sana nyendo zote za kiongozi wa Uamsho, Shekhe Farid ikiwamo kuhusishwa kwake na mtandao wa Al-Qaeda,” alisema.
Alisema licha ya kiongozi huyo na wenzake sita kuwa rumande, lakini uchunguzi wa kujua nyendo zao pamoja na uhusiano wake na taasisi za nje ya nchi kwa sasa unafanywa.
Aidha, alisema kiongozi huyo na wenzake wanatazamiwa kufikishwa tena katika Mahakama ya Mwanakwerekwe mjini hapa kwa ajili ya kusikilizwa shauri lao la dhamana kuhusu tuhuma za kufanya fujo na uchochezi.
“Maandalizi ya Polisi kufikishwa mahakamani kwa kiongozi wa Uamsho na wenzake yamekamilika na kusisitiza ulinzi mkali umewekwa katika maeneo yote jirani na mahakama hiyo,” alisema.
Viongozi saba wa Uamsho walifikishwa katika Mahakama ya Mwanakwerekwe Jumatatu wakituhumiwa kufanya fujo na uchochezi na kuhatarisha amani.
Viongozi hao ni Mselem Ali Mselem, Khamis S. Khamis, Mussa Juma Issa, Shekhe Azan Khalid Hamdani, Suleiman Juma na Hassan Bakari.
Mapema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imevitaka vyombo vya ulinzi kufanya uchunguzi wa kina kujua sababu zilizosababisha Shekhe Farid kutoweka huku akidai kutekwa nyara na kusababisha kuibuka kwa fujo.
Akitoa tamko la SMZ kuhusu suala la madai ya kutekwa nyara kwa Shekhe Farid na baadaye kuibuka kwa fujo zilizosababisha vifo vya wananchi na askari Polisi katika Baraza la Wawakilishi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud alisema uchunguzi wa kina unahitajika kufanywa ili kujua sababu zote.
“Tumeviagiza vyombo vya Dola kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha fujo zilizosababisha hasara kubwa na upotevu wa maisha ya wananchi,” alisema.
Alisema SMZ kamwe haitavumilia aina zozote za vitendo vinavyohatarisha amani na utulivu kiasi ya kutishia kuvurugika kwa uchumi wa nchi.
Aidha, aliviagiza vyombo vya ulinzi kudhibiti vitendo vya fujo vinavyofanywa na baadhi ya vikundi vya watu ikiwamo vijana wanaovamia wananchi na kupora mali zao.
Alisema kama Serikali itaendelea kuvumilia na kulea vitendo vya aina hiyo vinavyosababisha vurugu, uchumi wa Zanzibar na amali iliyopo utavurugika moja kwa moja na kutoweka.
“Serikali kamwe haitavumilia vurugu za aina hii ambazo zinahatarisha maendeleo ya sekta ya utalii huku sekta hiyo ikiwa kiongozi wa uchumi wa nchi,” alisema Aboud.
Hivi karibuni kulijitokeza uvunjifu wa amani visiwani hapa baada ya kuibuka vikundi vinavyovamia makanisa na kufanya uharibifu kwa kuvunja na kuchoma moto mali kwa kisingizio cha kulipiza kisasi kidini.
Kwa visiwani hapa hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya wafuasi wa Uamsho kusababisha ghasia kubwa wakidai kuwa Shekhe Farid ‘ametekwa na Polisi’, wakitaka aachiwe. Polisi ilikanusha madai hayo.
Ilifafanua kuwa kiongozi huyo wa Uamsho hakutekwa na wala vyombo vya usalama nchini havina sababu yoyote ya kumteka au kumkamata kisiri, kwani vinafanya kazi zake kwa uwazi, weledi na kwa mujibu wa sheria. Kama wangetaka kumkamata wasingemvizia na kumkamata kisiri.
Vurugu za wafuasi wa Uamsho zilisababisha kifo cha askari wa Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) F.2501 Koplo Saidi Abdrahamani Juma (41) ambaye alivamiwa na kupigwa. Chanzo cha vurugu hizi ni uchochezi mkubwa uliofanywa na viongozi wa kundi hilo, akiwamo Shekhe Farid.
Farid ambaye yuko rumande anadaiwa kuendesha mihadhara yenye kupandikiza mbegu za chuki, uhasama na uchochezi baina ya Watanzania wa Bara na Visiwani, na baina ya Wakristo na Waislamu.
Amekuwa akifanya hivyo katika misikiti na sehemu mbalimbali za Zanzibar.
Kwa mujibu wa habari zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari jana, Shekhe Farid ana asili ya Yemen, ambako wazazi wake walizaliwa kabla ya kuingia nchini na haijathibitika kama alikana uraia wa Yemen kama sheria ya Uhamiaji inavyotaka ili awe raia wa Tanzania.
Madai zaidi yaliyopo ni kwamba Shekhe Farid alipata kuajiriwa na Jeshi la Qatar lakini akafukuzwa kwa sababu za kiafya.
Hatua ya Polisi Zanzibar kumchunguza Shekhe Farid kwa tuhuma za kuhusiana na al Qaeda zinato-kana na madai kuwa alipata kushiriki mafunzo ya mtandao huo katika nchi tatu Arabuni ikiwamo Yemen.
"Huyu ana ujuzi wa kigaidi na hata kitendo chake cha kujificha na kudai katekwa, ni uongo na mbinu zake za kigaidi ili kuchochea ghasia na machafuko nchini," kilisisitiza chanzo cha habari kilichokaririwa na vyombo hivyo vya habari.
Shekhe Farid alikamatwa na kufikishwa mahakamani Oktoba 22 na viongozi wenzake wengine wa Uamsho baada ya kujitokeza kutoka mafichoni alikokuwa.
Wakati kukiwa na habari hizo kumhusu Shekhe Farid, ziko pia taarifa kwamba miongoni mwa wanaotuhumiwa sambamba naye kuna mmoja ambaye anadaiwa kuwa mwakilishi wa kikundi cha kiislamu cha Boko Haram cha Nigeria, akikiwakilisha katika Afrika Mashariki, kutokea Mombasa, Kenya.
Nchini wafuasi wake wanadaiwa kutumia jina la Hizb Tahrir na alipata kutambulishwa jijini katika viwanja vya Magomeni miaka takriban miwili iliyopita na wamekuwa na mkakati wa kuchoma makanisa na baa.
Kikundi cha Boko Haram kimekuwa ‘mwiba’ kwa Serikali ya Nigeria ambako kimekuwa kikishiriki kuchafua hali ya amani nchini humo kwa kushambulia makanisa na shule kwa mabomu.
Hata hivyo vikosi vya Serikali vimekuwa vikiendesha msako dhidi ya wapiganaji wa kikundi hicho na kufanikiwa kuua baadhi ya viongozi wake na wengine kuwatia mbaroni.
Boko Haram mbali na mashambulizi hayo, imekuwa ikipiga vita elimu ya Magharibi na kusisitiza matumizi ya sharia.

No comments:
Post a Comment