Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) wa Mkoa huo, Shekhe Abdulkarim Jonjo, amejeruhiwa na mlipuko unaosadikiwa kuwa wa bomu lililotegwa nyumbani kwake katika eneo la Esso.
Shekhe Jonjo alijeruhiwa na mlipuko huo saa 6.30 usiku wa kuamkia jana chumbani kwake eneo la Sokoni One, Esso, jijini humo ambapo pia chumba hicho kiliharibiwa baada ya kupata tundu kubwa ukutani.
Akisimulia kisa hicho katika wadi ya majeruhi ya Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru alikolazwa, Shekhe Jonjo alisema alifika nyumbani kwake juzi saa moja usiku umeme ukiwa umekatika.
Alisema aliingia ndani na baada ya muda mfupi, alipitiwa na usingizi lakini ilipotimu saa 4 usiku umeme ulirudi ndipo aliposhituka na kuamka kuchaji simu yake ya mkononi.
Baada ya kuacha simu hiyo, alisema aliendelea na usingizi na ilipotimu saa 6 usiku, ghafla aliona kitu kinawaka chumbani mwake.
Shekhe Jonjo alisema alishituka na kujiuliza ni nini akaenda kukishika ndipo kilipomlipukia na kumsababishia majeraha usoni, machoni, mkononi na kifuani.
Alisema baada ya mlipuko huo, alipoteza fahamu kwa muda na alipozinduka kwa sababu alikuwa peke yake kwa kuwa familia yake ilikwenda Tabora msibani, alipata akili ya kwenda kufungua mlango na kuomba msaada kwa majirani ambao walimwahisha hospitalini kupata matibabu zaidi.
"Nilikuwa peke yangu usingizini na niliposhituka niliona kitu kinawaka kama utambi nikajiuliza ni kitu gani ndipo nilipokwenda kukishika, kikanilipukia, ukweli nimepoteza damu nyingi na ninasikia maumivu," alisema.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mount Meru, Dk Ijosia Mlay alisema walimpokea Katibu huyo juzi usiku akiwa na maumivu ingawa si makubwa sana na hakuvunjika sehemu yoyote.
"Tunaendelea kumpa huduma lakini hajapata majeraha makubwa ni ya kawaida ila ameumia usoni, kifuani na baadhi ya sehemu za mwili lakini majeraha ni ya kawaida na si makubwa," alisema Dk Mlay.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo jana alifika hospitalini kumjulia hali na kumpa pole na kwenda nyumbani kwa Katibu huyo na kuwasihi wakazi wa Arusha kuacha kuingiza tukio hilo na masuala ya dini kwani ni mapema kutoa majibu.
Alisema tayari timu ya wataalamu wa milipuko ya Polisi na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) imeundwa kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama na watakapomaliza kuchunguza, majibu yao yatatoa taswira ya tukio hilo lililogubikwa utata.
"Tukio hili ni la utata kwani kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa wataalamu wa JWTZ na Polisi mlipuko wa bomu ulitokea ndani ya chumba cha Shekhe Jonjo na si nje hivyo ni mapema kusema aina ya bomu au aliyefanya hivyo, tusubiri uchunguzi," alisema.
Mmoja wa wataalamu wa JWTZ ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini, alisema mlipuko unavyotokea kama ungekuwa nje lazima moshi ungeonekana kwa nje lakini ulitokea ndani ndio maana chumbani kwa Shekhe Jonjo kulikutwa na moshi na nyufa.
“Kama mlipuko huu ungetokea nje lazima shimo lingekuwa dogo na kwa ndani likawa kubwa, lakini hili lina utata kwani kwa jinsi tunavyoona, mlipuko huu umeanzia ndani kwa kuwa kuna shimo dogo na nje ya dirisha lake katika chumba anacholala kunaonekana shimo kubwa," alisema mtaalamu huyo.
Mmoja wa majirani wanaoishi karibu na nyumba anayoishi Shekhe huyo, Mama Husna alikiri kusikia mtikisiko saa 6:30 usiku kwenye nyumba yao wakahisi ni majambazi.
Alidai wakati wanapigiana simu, ndipo walipogundua kuwa nyumba anayoishi Shekhe Jonjo pametokea mlipuko huo ingawa hawajui bomu hilo ni la aina gani.
Mpangaji anayeishi na Jonjo, Hillary Musa alisema alisikia mtikisiko katika nyumba wanayoishi yeye na wapangaji wenzake akiwamo Shekhe huyo na alipotoka nje alidhani ni shoti ya umeme, lakini ghafla alimwona Shekhe Jonjo akihitaji msaada ndipo walipomwuliza kulikoni, naye aliwaeleza ilibidi waombe msaada kwa majirani na kumkimbiza hospitalini.

No comments:
Post a Comment