Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba. |
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limewatia mbaroni watu watano kutoka Dar es Salaam wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow akiwemo anayedaiwa kuwa kinara wa mauaji hayo.
Aidha linawashikilia watu wengine watano wa jijini hapa ambao wanahojiwa juu ya mauaji ya kamanda huyo.
Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert Manumba aliwataja watuhumiwa hao ambao wanadaiwa na Polisi kuwa kabla ya mauaji hayo walifanya uporaji katika maeneo mengine ni pamoja na Muganizi Michael Peter (36) mkazi wa Isamilo ambaye alikiri mwenyewe kumuua kwa risasi.
Wengine ni Chacha Waitara Mwita (50), Magige Mwita Marwa, Bugazi Edward kusota na Bhoke Mara Mwita (42) ambao walikamatwa jijini Dar es salaam baada ya kuwekewa mtego kwa msaada wa wananchi.
Manumba alisema majambazi hao kabla ya kufanya mauaji hayo jijini mwanza walifanya uporaji katika maeneo mbalimbali majira ya saa 4 na 6 na kwamba wakiwa Dar es Salaam pia walifanya matukio ya uporaji,
Manumba ambaye alikuwa akitoa taarifa katika kikao kilichomshirikisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, Said Mwema alisema baada ya kuwakamata wauaji hayo pia wamefanikiwa kukamata bunduki mbili ikiwemo shotgun iliyotumika katika mauaji ya RPC pamoja na
ya aina Pump action ambazo zote zilipatikana jijini Dar es salaam zikiwa zimechimbiwa.
Alisema kupatikana kwa wauaji hao kunatokana na jeshi hilo kujipanga katika makundi yakiwemo intelijinsia, mahojiano na watuhumiwa wa wizi kwa kutumia mitandao ambavyo vilisambaa katika mikoa yote ya kanda ya ziwa na mingineyo ili wasitoe nafasi kwa wahalifu kukimbia.
Manumba alisema bado jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ambapo watu wawili waliohusika katika tukio hilo bado wanasakwa.
Wanaoshikiliwa jijini Mwanza kwa mahojiano ni pamoja na Mwalimu Doroth Moses Lyimo aliyekuwa na RPC wakati mauaji yakitokea, Felix Felician Minde (50), Philemon Felician (46) maarufu kama Fumo, Bahati Agustino Lazaro (28) na Amos Magoto (30) maarufu kama Bonge.
Naye IGP, Mwema alisema jeshi la polisi halitasita kumchukulia hatua mtu yeyote anayefanya uhalifu, hujuma na uchochezi kwa kisingizio chochote ili kupunguza uhalifu hapa nchini.
Alisema kifo cha RPC Barlow kimewafanya kuwa imara na kukuza uweezo wao wa kulinda wananchi na viongozi mbalimbali serikali.
Hata hivyo alisema uchunguzi wa kifo cha RPC Barlow bado unaendelea kutokana na taarifa mbalimbali wanazoendelea kuzipokea kutoka kwa raia wema na kuwashukuru wananchi na vyombo vya habari kwa ushirikiano waliounyesha tangu mauaji hayo yatokee.
IGP Mwema aliwasili jijini Mwanza jana mchana na kukutana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa, kisha alizungumza na askari polisi wapata 500 katika ukumbi wa halmashauri ya jiji na kisha alizungumza na vyombo vya habari ambapo alisema madhumuni ya ujio wake ni pamoja na kukagua na kufanya tathmini ya tukio la kuuawa kwa kamanda Barlow pamoja na kuangalia hali ya usalama ya mkoa.
Marehemu Kamanda Barlow aliuawa usiku wa Oktoba 12 majira ya kati ya saa 7 na 8 usiku katika eneo la Kitangiri, kona ya Bwiru baada ya kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.

No comments:
Post a Comment