KAMANDA WA POLISI MWANZA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI...

Habari zilizotufikia zinasema kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP), Liberatus Barlow ameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.
Taarifa kutoka Mwanza ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, zinasema kuwa Kamanda Barlow aliuawa baada ya kumrudisha dada yake kutoka katika kikao cha harusi ya ndugu yao huko Kitangili.
Tutawaletea taarifa kamili kuhusu tukio hilo baadaye.

No comments: