AFA BAADA YA GARI LAKE KUPINDUKA NA KUTUMBUKIA BAHARINI...

Mtu mmoja amekufa baada ua gari alilokuwa akiendesha kupinduka na kujibamiza kwenye mwamba umbali wa futi 400 kabla ya kutumbukia baharini.
Wafanyakazi wa boti za uokoaji walikwama kumpata dereva akiwa hai chini ya mwamba baada ya kutupwa nje ya gari wakati lilipoporomoka kutoka ufukweni huko East Sussex juzi jioni.
Alikimbizwa hospitalini na helikopta ya doria ukanda wa pwani baada ya boti za uokoaji kukwama baada ya kukumbana na hali mbaya ya hewa kuweza kufika eneo la tukio, lakini akafariki baadaye.
Polisi kwa sasa wanachunguza jinsi na kwanini gari hilo lilijibamiza kwenye mwamba.
Gari hilo liliporomoka majira ya Saa 12:23 jioni ya juzi.
Boti za uokoaji za Eastbourne zilipambana na mawimbi makali huku giza likianza kuingia kuweza kufika ufukweni, ambako walimkuta dereva huyo akiwa bado hai.
Madaktari wa boti za uokoaji walihamishiwa eneo la pwani kusimamia huduma ya kwanza na kuimarisha hali yake ya kiafya.
Baadaye alihamishwa kwa kutumia boti za madaktari kwenda kwenye helikopta ya doria na kupelekwa moja kwa moja katika Hospitali ya Riyal Sussex County mjini Brighton.
Lakini msemaji wa polisi wa Sussex alithibitisha kwamba mwanaume huyo alifariki hospitalini muda mfupi baadaye.
Msemaji wa Eastbourne RNLI, Bob Jeffery alisema: "Mtu huyo alitupwa nje ya gari lake na tulipofika pale tulikuwa tunatarajia mabaya lakini tulimkuta akiwa hai na kwa bahati tuliongozana na daktari.
"Ilikuwa ni hali ya umauti katika giza na kukiwa na mawimbi makali na mmoja wa wafanyakazi alilazimika kuogelea pwani kuweza kuifikia boti ndani.
"Zoezi hilo lilichukua takribani masaa matatu na nusu huku helikopta ya doria ikilazimika kurudi kuwachukua wafanyakazi waliokwenda pwani."

No comments: