CHEKA TARATIBU...

Mlevi kaingia kanisani Jumapili na moja kwa moja akaenda kukaa kando ya mrembo mmoja. Wakati ibada ikiendelea yule Mlevi akamwambia yule mrembo, "Niazime simu yako mara moja nitume meseji!" Yule Mrembo kwa mshangao akajibu, "Hivi hujui kama tuko kwenye ibada?" Mlevi kwa ukali akasema, "Kama ulijua hilo kwanini sasa ukaingia nayo?" Kasheshe...

No comments: