KUSHOTO: Nyumba yalikofanyika mauaji hayo. JUU: Natalia Woolley. CHINI: Winston Fernandez. |
Mwili wa Winston Fernandez mwenye miaka 69, haukuweza kugundulika kwa zaidi ya mwezi baada ya changudoa wa Kirusi, Natalia Woolley kumpiga hadi kufa, ilidaiwa mahakamani hapo.
Changudoa huyo ambaye hutoza Pauni za Uingereza 600 kwa usiku mmoja, ambaye amejielezea kwenye mtandao kama 'anayetamanisha wanaume wote na mwenye mvuto wa kipekee', anasemekana alifikia hatua hiyo baada ya kuingia kwenye mzozo kuhusu huduma gani angeweza kutoa.
Wazee wa mahakama walielezwa alirudiarudia kumpiga mteja wake kabla ya kukata nyaya za simu na kumtelekeza akisubiria kifo.
Mwendesha mashitaka William Saunders alidai Natalia alirudirudia kumpiga mstaafu huyo na kumwacha akiwa amekufa au kufa taratibu kutokana na majeraha yaliyotapakaa mwili mzima, ikiwa ni pamoja na mbavu 17 zilizovunjika na mifupa miwili iliyovunjika katika sehemu ya mwanzo ya koromeo inayohusika na kutoa sauti.
Saunders aliongeza: "Uchunguzi ulionesha alikuwa amepigwa hadi kufa. Kwa kupigwa namaanisha ngumi na mateke.
"Majeraha haya yanawezekana yalimfanya ashindwe kuinuka, katika maumivu ya kawaida, na pengine alikuwa na matatizo pia katika upumuaji."
Winston alianza kulewa na kutembea na wasichana baada ya kifo cha mkewe, Joan miaka 12 iliyopita, Mahakama ya Guildford ilielezwa.
Alipanga miadi na Natalia mara tatu zilizopita kupitia wakala na hata kuandika katika mtandao kumsifu kutokana na 'masaa manane ya huduma yake ya kustaajabisha'.
Aliandika: "Yote safi, si ya kawaida. Ni furaha yangu kuwa nawe kila wakati! Siishi hamu kwako, nitatumia maisha yangu yote kwako!!"
Wazee wa mahakama ilielezwa wawili hao walianza kupigana wakati walipokutana nyumbani kwa Winston mjini Epsom, huko Surrey, baada ya changudoa huyo kuwasili majira ya Saa 1:30 usiku wa Januari 16, mwaka huu. Natalia baadaye aliwaeleza polisi alimshambulia wakati akijilinda baada ya Winston kumsukuma kitandani na kujaribu kumlazimisha kufanya mapenzi bila ridhaa yake.
Alidai kuwa Winston akiwa amelewa alimbana na kujaribu kumpiga kwa chupa kichwani.
Lakini Saunders alisema hii sio sababu ya majeraha ya Winston, ambayo yalisababishwa na kutumika nguvu ya ziada.
Natalia alikana mashitaka hayo. Kesi hiyo bado inaendelea.
No comments:
Post a Comment