MAZISHI YA MHASHAMU ASKOFU PASCAL KIKOTI NDANI YA KANISA LA MTAKATIFU IMAKULATA...

Mfululizo wa matukio katika ibada ya mazishi ya Askofu wa Kwanza wa Jimbo Katoliki la Mpanda, Mhashamu Pascal Kikoti ndani ya Kanisa la Mtakatifu Maria Imakulata mjini Mpanda juzi.
Alipolala Mhashamu Askofu Pascal Kikoti.
Mafundi wakifunika kaburi la Mhashamu Pascal Kikoti.
Maaskofu wakiweka ishara ya msalaba juu ya kaburi la Mhashamu Askofu Pascal Kikoti.
Mwili wa Askofu wa Kwanza wa Jimbo Katoliki la Mpanda, Mhashamu Pascal Kikoti ukiingizwa kaburini.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Askofu wa Kwanza wa Jimbo Katoliki la Mpanda, Mhashamu Pascal Kikoti kabla ya mazishi.
Mapadri wakiwa wamejipanga kando ya jeneza lenye mwili wa Mhashamu Askofu Pascal Kikoti.
Mhashamu Polycarp Kardinali Pengo (kushoto) akiongoza ibada mbele ya jeneza lenye mwili wa Askofu wa Kwanza wa Jimbo Katoliki la Mpanda, Mhashamu Pascal Kikoti.
Kanisa la Mtakatifu Maria Imakulata mjini Mpanda ambamo amezikwa Mhashamu Askofu Pascal Kikoti.

No comments: