ATUMBUA PAUNI 50,000 CHAPCHAP KUKWEPA KUDAIWA NA MKEWE...

Baada ya Scott Brown kuchemsha akili zake za kushinda Pauni za Uingereza 50,000 katika Onesho maarufu la 'Deal or No Deal', alibainisha kwamba mkewe waliyetengana naye hawezi kupata hata senti.
Lakini miezi minne tu kabla ya onesho hilo la Televisheni kuoneshwa na kugundua kuhusu nyota yake ya jaha, baba wa watoto wawili alijua fika analazimika kuzitumia pesa hizo haraka sana.
Scott mwenye miaka 33, mtengenezaji alama na mfitishaji alisema alitumia Pauni 15,000 kulipa madeni yake yote na mkewe, Rachel mwenye miaka 29, yaliyotokana na kadi ya malipo, mikopo na madeni katika akaunti za benki.
Baada ya kutenga kando takribai Pauni 2,000 kwa ajili ya ada ya kisheria kwa ajili ya talaka yake, alinunua nguo, wanasesere na vitu vya ndani kwa ajili ya watoto wao wawili wadogo.
Scott pia alitumia kiasi fulani kwa ajili ya 'kujifariji' baada ya kuwa amefukuzwa kazi kwa sababu ya 'mfadhaiko'.
Lakini amekiri alitumia sehemu kubwa ya kiasi kilichobakia 'kujirusha', ikiwamo kununua iPad, kwenda mapumzikoni nchini Mexico na kutumia Pauni 4,000 kununua gari aina ya Jaguar X-type kuukuu.
Sehemu yake ya mwisho zawadi ya ushindi wake ilimalizikamuda mfupi kabla ya siku yake ya mwisho aliyopewa ili kukamilisha malipo ya kozi yake ya masuala ya umeme, hivyo kumwezesha kuanza taaluma mpya.
Scott alikuwa sahihi kuhisi kwamba mkewe, ambaye alisema alidai talaka siku ya Krismasi mwaka jana baada ya kuwa ametuhumiwa kugundulika kuwa na mahusiano na dereva wa magari makubwa aliyefahamiana naye kupitia mtandao wa intaneti, angetaka mgawo wake wa fedha katika zawadi hiyo.
Mapema kabla ya kipindi hicho kutangazwa katika televisheni ya Channel 4, alikwenda mahakamani katika jaribio lililochelewa kuhakikisha anapata mgawo wake huo.
Kesi hiyo ilisikilizwa mbele ya Jaji wa Wilaya kwenye Mahakama ya Doncaster County Alhamisi iliyopita, pale Scott alipokuamriwa kutoa kimaandishi mchanganuo wa jinsi alivyotumia fedha hizo; zuio lililowekwa siku chache kabla likimwamuru kutotumia zaidi zawadi yake -ikiwa kuna chochote kilichosalia- kutengwa; na kesi hiyo ikaahirishwa.
Wawili hao, ambao walikuwa kwenye mchakato wa kuachana, hakuna aliyemtazama mwenzake wala kuzungumza wenyewe kwa wenyewe wakati wote wa kusikilizwa kesi hiyo.
Nje ya mahakama, Scott alieleza jinsi onesho hilo lililoendeshwa na Noel Edmonds, lililovyobadilisha maisha yake pale alipokuwa kwenye lindi la ufukara, akisema: "Sikutarajia kabisa kushinda kiasi kikubwa kama kile. Nilielezwa kwamba Rachel anaweza kudai chochote kutoka kwenye fedha hizi ndipo nikaamua, "Hapati hata senti moja'."
Scott alimuoa mshauri wa huduma za wateja, Rachel katika Jamhuri ya Dominica Septemba mwaka 2009.
Wawili hao tayari wamefanikiwa kupata mtoto mmoja ambayeana miaka sita sasa, na kukubaliana kupata mtoto mwingine, ambaye sasa ana miezi 22.
Familia hiyo ilikwenda kupanga nyumba kubwa karibu na Doncaster lakini madeni yao yakaanza kupaa kwa kasi.
Scott alisema mkewe alimweleza mwishoni mwa mwaka jana kwamba 'hampendi tena' na kwa wakati huo akijua kwamba alikuwa akielekea kwenye onesho hilo mwezi Aprili, Scott alihama kwenye nyumba hiyo na kwenda kulala sakafuni katika nyumba ya wazazi wake.
Alisema kwamba 'alikerwa mno' na mkewe, akisema: "Anawezaje kuwa na haki katika fedha hizi? Mke wangu ameshajitenga, siwezi kuwaona tena wanangu kila siku na nimepoteza kila kitu nilichovuna katika miaka yangu 11 ya kufanya kazi." Rachel aligoma kutoa maoni yoyote.
Katika 'Deal Or No Deal', mshiriki anachagua kasha moja kati ya 22 yaliyofunga lakiri lililofichwa kiasi kikubwa cha fedha zinazoanzia Senti 1 hadi Pauni 250,000, kisha kuondosha kasha moja baada ya jingine.
Scott alicheza kamari wa kukataa ofa za Pauni 22,000 na Pauni 13,000 kutoka kwa 'mtunza fedha' wa onesho hilo ili 'kukubali' na kutoendelea na mchezo, badala yake aliendelea hadi mwisho na kushinda Pauni 50,000 katika kasha lake.

No comments: