Wapenzi ambao wanadaiwa kuwa na mahusiano kabla ya ndoa wamepigwa mawe hadi kufa na kundi la askari wa Kiislamu linalotawala upande wa Kaskazini wa Mali.
Wawili hao vijana waliuawa hadharani kwenye mji mdogo usiofikika kirahisi wa Aguelhok, karibu na mpaka wa Kaskazini wa taifa hilo la Afrika Magharibi na Algeria, Jumapili iliyopita, msemaji wa kundi la Ansar Dine (walinzi wa imani) alisema.
"Watu wetu waliokuwa huko Aguelhok walitumia Sheria ya Kiislamu 'Sharia', Sanda Ould Bounama alisema Jumatatu iliyopita.
"Wote wawili walikufa pale pale bila kuhoji matumizi ya sheria hii. Hatutakiwi kumjibu yeyote kuhusu matumizi ya Sharia," alisema.
Watu wengi wanaoishi kaskazini mwa Mali kwa muda mrefu wamekuwa wakiishi Kiislamu, lakini wanakatishwa tamaa na ukali wa sharia unaotumiwa na wanaharakati wa Kiislamu umekuwa mchungu kwa waandamanaji katika miezi ya karibuni.
Ansar Dine na vikosi imara vya kivita, ikiwamo kundi lililojitenda kutoka Al Qaeda laMujwa, wameteka kundi la waasi la Tuareg na sasa kutwaa theluthi mbili ya kaskazini mwa jangwa la Mali, ikiwamo miji ya Gao, Kidal na Timbuktu.
Magharibi na Serikali za Afrika zinahaha kudhibiti machafuko huku wanasiasa katika mji mkuu Bamako wakiendelea kupigia kelele jinsi nchi inavyotakiwa kuongozwa baada ya mapinduzi ya mwezi Machi kumwondoa madarakani rais wa nchi hiyo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty Afrika, Paule Rigaud alisema: "Amnesty inalaani vitendo hivi vya kutisha na kuogofya vya mauaji kwa kupigwa mawe.
"Mauaji haya ni ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu unaofanywa na wapiganaji wanaotawala kaskazini ya Mali.
"Amnesty imeandaa taarifa ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyofanywa na makundi nchini Mali kwa watu kubadilika tabia kwa mujibu mafundisho yao na tafsiri za Uislamu.
"Tabia mpya zinazopiganiwa ni pamoja na aina ya mavazi kwa wote wanawake na wanaume, kufungia miziki yote isipokuwa miziki ya kidini na kupiga marufuku watu wa jinsia tofauti kama hawajaoana kukaribiana kwenye basi au kutembea mitaani pamoja."

No comments:
Post a Comment