Wapelelezi wanaochunguza kutoweka na kupotea mkurugenzi wa mafuta, Carole Waugh wamekuta mwili katika gereji moja iliyofungwa mjini London, Polisi wa Scotland Yard wamesema.
Polisi waligundua mwili katika gereji moja iliyoko huko Lime Court, New Malden, kusini magharibi mwa Lindon Alhamisi iliyopita kufuatia upelelezi wa polisi.
Mpelelezi Mkuu Inspekta John McFarlane, alisema Jumatano iliyopita kwamba walikuwa na kila sababu ya kuamini kwamba milionea huyo aliyepotea alikuwa hajaonekana akiwa hai tangu Aprili 16, mwaka huu.
Mara ya mwisho inayoaminika Carole alionekana awali ilidhaniwa kuwa ni katikati ya London Mei 4, mwaka huu lakini hii haijathibitishwa na polisi sasa wanaamini kwamba hajaonekana akiwa hai tangu Aprili 16. Hajawahi kupotea hapo kabla.
Kufuatia kupotea kwa Carole, kumeibuka mlolongo wa matukio mbalimbali ya uhalifu yanayohusishwa na akaunti ya benki ya Carole.
Mpaka sasa, watu 10 wamekamatwa kuhusiana na uchunguzi huo. Vitu kadhaa anavyomiliki havijulikani vilipo kwa sasa.
Faili la uchunguzi wa tukio hilo lilifunguliwa huko Sutton chini ya Mpelelezi Mkuu Inspekta John McFarlane wa Kikosi cha Upelelezi wa Mauaji ya Watu na Makosa Sugu (HSCC).
Kesi hiyo mwanzoni ilichukuliwa kama ya uchunguzi wa mtu aliyepotea na kwamba sasa imegeuka na kuwa ya uchunguzi wa mauaji.
McFarlane alisema: "Taarifa zimekuwa zikipokelewa ambazo ni mwendelezo wa upelelezi na sasa tunachukuliwa kupotea kwa Carole kama uchunguzi wa mauaji.
"Siwezi kuingia kwa undani zaidi kuhusu uasili wa taarifa mpya kwa sasa, hatahivyo, sasa tunaamini kwamba Carole hajaonekana akiwa hai tangu Aprili 16. Tangu wakati huo, umuhimu wa utekaji nyara wa shamba lake umechukua nafasi kuwa na thamani ya mamia ya maelfu ya Pauni.
"Zaidi ya ongezeko la uhalifu wa amali kuhusiana na akaunti ya benki ya Carole pia kuna vitu kadhaa binafsi anavyomiliki ambavyo kwa sasa havijulikani vilipo.
"Natoa picha za vitu kama vito vya Cartier, ambavyo vinashabihiana mno na alivyokuwa akivaa Carole, ambavyo kati ya vingi navyo havijulikani vilipo kutoka kwenye himaya yake.
"Vito vilivyopotea ni kama vifuatavyo: pete ya Cartier; kikuku cheupe cha dhahabu; kikuku cha njano cha dhahabu na mkufu wa njano wa dhahabu wa shingoni, ambavyo vyote vinafanana mtindo wake.
Wapelelezi walisema Carole, ambaye hapo kabla aliwahi kuishi nchini Libya, alikuwa akikutana na wanaume mbalimbali kupitia mtandao wa intaneti ikiwamo mitandao kadhaa ya kutongozana na walikuwa wakichunguza uwezekano kwamba alikuwa ameongozana na mtu.

1 comment:
Eνeгything iѕ veгу opеn
with a precisе claгificаtіon οf the iѕѕues.
It ωas defіnitely іnfοrmative.
Your ѕite is useful. Thanks for sharіng!
Ϻy web blog - payday loans online
Feel free to visit my weblog : Payday Loans
Post a Comment