CHEKA TARATIBU...

Jamaa mmoja kaingia baada ya kukuta mlevi kakaa kwenye meza ya pembeni huku chini ya meza akiwa kajilaza mbwa. Jamaa akamuuliza yule mlevi, "Samahani, huyu mbwa wako hawezi kuning'ata?" Mlevi akajibu kwa kifupi, "Hapana." Baada ya dakika kama kumi hivi mbwa akamrukia yule jamaa na kumng'ata mguu wake. Jamaa akamfuata yule mlevi kwa hasira na kusema, "Lakini nilikuuliza kuhusu huyo mbwa wako, unaona sasa alichonifanya?" Mlevi huku akiinuka na kuondoka akajibu, "Huyo sio mbwa wangu!" Duh...

No comments: