SAID BAHANUNZI, ATHUMANI IDDI 'CHUJI' WAONGEZWA KIKOSINI TAIFA STARS...


Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Kim Poulsen ameongeza wachezaji watatu kwenye kikosi chake cha wachezaji 21 aliowatangaza jana katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa ajili ya mechi ya kirafiki itakayochezwa ugenini Agosti 15 mwaka huu.
Miongoni mwa wachezaji walioitwa, yupo mfungaji bora wa michuano ya Kombe la Kagame iliyomalizika hivi karibuni, Saidi Bahanunzi na Athumani Iddi ‘Chuji’ wa Yanga pamoja na Ramadhani Chombo wa Azam.
Wachezaji hao watatakiwa kuripoti kambini kwenye hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam, Jumatano ijayo tayari kwa mazoezi yatakayoanza siku inayofuata. 
Kikosi kamili:
Makipa: Deogratias Munishi, Mwadini Ally,  (Azam) na nahodha wa kikosi hicho  Juma Kaseja (Simba). 
Mabeki: Nahodha msaidizi Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba). 
Viungo: Athumani Iddi, Frank Domayo (Yanga), Haruna Moshi, Mwinyi Kazimoto, Ramadhan Singano (Simba), Mrisho Ngassa, Ramadhan Chombo, Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar). 
Washambuliaji: John Bocco (Azam), Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Saidi Bahanunzi, Simon Msuva (Yanga).

No comments: