Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Asiye na Wizara Maalumu, Profesa Mark Mwandosya jana aliingia bungeni kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje kwa zaidi ya mwaka mmoja kutokana na kuugua, huku akisema mkono wa Mungu umefanya kazi.
Profesa Mwandosya aliingia ukumbini muda mfupi kabla ya Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kuanza kusoma makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Wizara hiyo mwaka 2012/13.
Lakini wakati Dk Mwakyembe akianza kusoma hotuba yake, ghafla wabunge walianza kupiga meza kushangilia kiasi cha baadhi kutotatumbua kwa haraka nini kilichokuwa kinaendelea, hivyo Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama kumtaka Dk Mwakyembe asimame kwanza kusoma hotuba yake.
Mhagama alisema ni vizuri kwa wananchi waliokuwa wanafuatilia mjadala wa Bunge kwa njia ya televisheni wakaelewa shangwe hizo za wabunge ilikuwa ni nini na kufafanua kuwa furaha ya wabunge ni kuingia tena bungeni kwa Profesa Mwandosya na kusema wanamkaribisha sana.
Lakini muda mfupi baada ya tukio hilo, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye alikuwa ndiye Mkuu wa Shughuli za Serikali bungeni, Samuel Sitta, alisimama na kutoa taarifa kwa Mwenyekiti kwamba ni vyema Profesa Mwandosya akapewa nafasi ya kuzungumza japo kidogo, kauli ambayo ilitekelezwa.
Akizungumza, Profesa Mwandosya alisema alijisikia faraja kupata nafasi hiyo kwani wakati anaugua alikuwa akiomba siku moja apate nafasi ya kujumuika na wenzake japo kwa muda mfupi ili azungumze nao.
Alisema kwa kipindi cha mwaka mmoja alichokuwa mgonjwa amejifunza mambo mengi, lakini kubwa ni kuwa kuna haja ya Serikali kuwekeza zaidi katika sekta ya afya kwa kuwa afya ni kila kitu kwa mwanadamu na kutania kuwa ukiwa huna afya nzuri, hata Mwongozo wa Spika huwezi kuomba bungeni.
Alisema katika kupona kwake kwa haraka anaona mkono wa Mungu una nafasi kubwa na kusisitiza kuwa anamshukuru zaidi Rais Jakaya Kikwete kwa kuwa na nafasi kubwa katika afya yake na hata kuhakikisha anenda India kutibiwa.
Alisema Rais alimtaka ajali kwanza afya yake badala ya kufikiria vijiji visivyokuwa na maji (wakati anaanza kuumwa alikuwa Waziri wa Maji) na kuwa hilo lilimfariji sana na pia kutaja orodha ya viongozi mbalimbali waliomtakia heri kila wakati kipindi chote cha kuugua.
Aliwataja baadhi kuwa ni Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Seif Shariff Hamad na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd na wabunge wote.
Aliwashauri wabunge wajenge utaratibu wa kupima afya kila mara na kuongeza kuwa yeye kwa karibu miaka 45, hajawahi kulazwa hospitalini na aliamini ana afya njema kwa vile ni mtu wa mazoezi.

No comments:
Post a Comment