Armstrong amefariki kufuatia matatizo yaliyosababishwa na taratibu za mishipa ya damu kwenye moyo, familia yake imeeleza katika taarifa. Haikufahamika alifia wapi hasa.
Taarifa hiyo kutoka kwa familia ya Armstrong ilieleza katika sehemu mojawapo, "Wakati tukiomboleza kuondokewa na mtu wetu mwema sana, pia tunasherehekea maisha yake ya ajabu na matumaini kwamba itasaidia kama mfano kwa vijana duniani kote kufanya kazi kwa bidii ili kukamilisha ndoto zao."
Armstrong aliongoza chombo cha Apollo 11, ambacho kilitua kwenye mwezi Julai 20, 1969. Katika masaa yake matatu akitembea kwenye udongo wa mwezini, aliwasiliana kwa njia ya radio, "Hiyo ni hatua moja ndogo ya mtu, hatua kubwa kwa ubinadamu."
Armstrong alifunga ndoa na mkewe wa sasa Carol mwaka 1999 na kuishi katika kitongoji cha Cincinnati huko Indian Hill. Alikaa kwa muda mwingi mbali na macho ya watu katika miaka ya hivi karibuni.
Kamera zilifanikiwa kumnasa Armstrong mara moja tu, nayo ilikuwa mwaka 2009 ambapo aliulizwa ni nyota gani angependa kumuona akienda kwenye mwezi na kwanini saini zake zinagharimu fedha nyingi mno!
No comments:
Post a Comment