Hili ni tukio ambalo mnyanyua uzito wa Misri, Khalil Mahmoud Abir Abdelrahman alipoangukiwa na chuma kisha kutupwa sakafuni wakati akijaribu kunyanyua uzito wa kilo 151 katika Michezo ya Olimpiki inayoendelea mjini London.
Mnyanyua uzito huyo mwenye urefu wa futi 5"3 alikuwa akijaribu kutetea uongozi wake katika mchezo huo baada ya kufanya vema katika mzunguko wa kunyanyua uzito wa chuma cha kilo 75.
Maumivu yake ya kutolewa kwenye michuano hiyo yamekuja baada ya mnyanyua uzito wa Korea Kusini, Jaehyouk Sa kulazimika kujitoa mashindanoni Jumatano baada ya kiwiko chake kuvunjika na kugeukia nyuma wakati akijaribu kunyanyua chuma cha uzito wa kilo 162.
Akiwa anaonekana kama kajiandaa vilivyo, Khalil alianguka kinyumenyume kutoka sehemu aliyokuwa kasimama na kisha chuma hicho kumgonga kifuani na kumlazimisha kulala sakafuni.
Timu ya madaktari ilimwendea na kumpa huduma ya kwanza baada ya dakika kadhaa alikuwa tayari kapatiwa msaada na kukimbizwa kwenye Kituo cha Afya cha London ExCeL akiwa kwenye kiti maalumu cha kubebea wagonjwa.
Lilikuwa jaribio lake la mwisho kunyanyua uzito akichuana na mshindi Svetlana Podobedova kutoka Kazakhstan, Natalya Zabolotnaya wa Urusi aliyenyakua medali ya fedha na Iryna Kulesha wa Belarus aliyenyakua medali ya shaba kwa kushika nafasi ya tatu.
Mapema wiki hii kumekuwa na matukio kama hayo ya kuumia katika unyanyuaji uzito pale bingwa mtetezi kwa kundi la uzito wa kilo 77, Jaehyouk Sa alipokumbwa na dhahma hiyo.
Mchezaji huyo kutoka Korea Kusini alikimbizwa hospitalini baada ya jaribio lake la pili kuishia kwenye ajali hiyo.

No comments:
Post a Comment