Zawadi ya Dola za Kimarekani 300,000 hatimaye imepata mwenyewe usiku wa kuamkia leo baada ya siku 91 za mikikimikiki na mbinde za hapa na pale katika shindano la Big Brother Africa Stargame.
Mshiriki kutoka Afrika Kusini, Keegan ndiye aliyeibuka kidedea baada ya kuwashinda washiriki wengine watano waliofanikiwa kumaliza siku zote 91 za kukaa kwenye jumba hilo ambalo mwaka huu mwanzoni liligawanywa katika sehemu mbili, yaani Upville na Downville, kabla ya washiriki hao kuunganishwa katika jumba moja hadi ilipofikia tamati usiku wa kuamkia leo.
Presha ilizidi kupanda kabla ya mwongozaji shughuli hiyo TK kumtangaza mshindi, huku kukiwa kumebaki washiriki wawili tu mjengoni humo, Keegan na Prezzo kutoka Kenya, baada ya washiriki wengine Lady May, Talia, Kyle na Wati kutolewa mapema jana katika shindano lililokuwa likioneshwa na DStv kupitia chaneli yake ya Africa Magic namba 198.
Hii ni mara ya kwanza kwa Afrika Kusini kuibuka washindi wa shindano hilo baada ya kutoka kapa tangu kuanzishwa kwa shindano hilo ambalo linafanyika katika ardhi yao.
Japo safari hii Tanzania haikufua dafu baada ya washiriki wake wawili, Edward na Hilda kutolewa katika wiki ya kwanza tu, miaka michache iliyopita iliweza kufanya vizuri kupitia kwa Richard aliyeibuka kidedea na kufuatiwa Mwisho Mwampamba aliyeshika nafasi ya pili katika mwaka uliofuatia.
Katika shindano la mwaka huu, washiriki wawili wa Afrika Mashariki walifanya vema kwa kumaliza siku zote 91 ndani ya jumba hilo. Mbali na Prezzo wa Kenya, Kyle kutoka Uganda naye alifanikiwa kumaliza siku zote humo.

No comments:
Post a Comment