AFA KWA MSHITUKO WA MOYO KWENYE MCHEZO WA KUZUNGUSHWA HEWANI...

Mama ameanguka na kufariki muda mfupi baada ya kuzungushwa kwenye gurudumu linalozunguka hewani.
Carla Knight alipatwa na mshituko wa moyo mapema baada ya gurudumu hilo kuanza kuwazungusha watu hewani umbali wa futi 70 kutoka ardhini huku wakitazama gondola hiyo inayozunguka.
Mama huyo wa watoto wawili mwenye miaka 42 alikufa papo hapo aneo la tukio licha ya juhudi za watu wa huduma ya kwanza, na madaktari waliokuwa kwenye mapumziko kujaribu kuokoa maisha yake.
Mchezo wa gurudumu hilo lenye thamani ya Dola za Marekani milioni 1, ambayo huwavutia watu wengi 'kuweza kushuhudia jicho la dhoruba', ilifungwa kwa masaa kadhaa baada ya ajali hiyo huko Drayton Manor Theme Park, mjini Tamworth, Staffordshire asubuhi ya Ijumaa iliyopita.
Lissy Goodyear mwenye miaka 17 alishuhudia tukio hilo. "Walisimamisha gurudumu hilo kuweza kumtoa na kumlaza sakafuni," alisema.
"Niliwaona madaktari wakijaribu kuzindua mapigo ya moyo wake kwa kutumia mashine ya CPR.
"Sidhani kama kuna la zaidi wanaloweza kufanya. Ilikuwa inasikitisha mno kutazama."
Carla, ambaye anaishi huko Barwell, mjini Leicester, anafanya kazi kama mwangalizi wa watoto wenye mazingira magumu kusoma katika Shule ya Dorothy Goodman iliyoko Hinckley, mjini Leicestershire.
Imefahamika kwamba siku hiyo alikuwa na mmoja wa wanafunzi wake kutoka shule hiyo na hakuwa na watoto wake wawili, Rosie mwenye miaka 14 na Aaron mwenye miaka 17.
Juzi, Rosie alituma ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook akieleza kwa kifupi 'Kalale Pema Peponi Mama Nakupenda'.
Aaron alisema: "Hakuwa na mwanafamilia yeyote wakati akifariki.
"Alikuwa akifanya alichoweza kufanya vema na kufurahia mno kazi yake." Aliongeza: "Tafadhali heshimuni ufaragha wetu kuhusu maumivu haya ya kumpoteza mama yangu."
Carla alifahamika kwa msaada wake kwa michango mbalimbali ya hisani ikiwamo katika tiba ya Kansa ya Matiti na Msaada wa Kanda wa Macmillan.
Jirani yake alizungumzia mshituko alioupata kufuatia kifo hicho cha ghafla. Mwanamke mmoja alisema: "Carla alikuwa mama aliyejitolea na aina ya mwanamke mwenye kujali.
"Familia yake itakuwa imeharibiwa, alikuwa mwenye bidii sana kwa watoto wake. Ni janga kubwa mno.
"Hakuna anayestahili hilo, hasa mtu ambaye ni kijana sana."
Mwenzake kutoka Shule ya Dorothy Goodman alisema: "Umekuwa ni mshituko mkubwa sana kwa kila mmoja anayefanya kazi kwenye shule hii.
"Carla alikuwa mwenye upendo sana na mtu mwenye kujali na hakika atakumbukwa na kila mfanyakazi na wanafunzi ambao walimfahamu."
Polisi wa Staffordshire waliitwa eneo la tukio majira ya saa 5:35 asubuhi Ijumaa, na kusema hakuna dalili zozote za kumshuku yeyote.
Colin Bryan, Mkurugenzi Mkuu wa Drayton Manor Park, alisema fikra zake ziko na familia ya Carla na marafiki zake.
Drayton Manor Theme Park imekuwa ikivutia zaidi ya watu milioni moja kwa mwaka.
Oktoba mwaka 2010, wapenzi wa mchezo wa kuzunguka kwenye mashine ya G-Force Roller Coaster kwenye Drayton Manor Theme Park walilazimika kuokolewa baa da ya kunasa kwa zaidi ya saa nzima pale gurudumu hilo liliposimama ghafla. Gurudumu hilo lilifungwa kwa ajili ya ukaguzi wa usalama wake.

No comments: