Utawala wa Michael Phelps kwenye michezo ya Olimpiki imefikia ukingoni kufuatia kumaliza akiwa katika nafasi ya nne kwenye mashindano ya kuogelea ya Mita 400, hivyo kutoka mikono mitupu bila kupata medali yoyote.
Mmarekani Ryan Lochte ndiye aliyenyakua medali ya dhahabu katika mashindano hayo ikiwa medali ya kwanza kwa Marekani mpaka sasa kwenye Michezo ya Olimpiki kmwaka huu.
Phelps alifuzu kwa fainali hizo baada ya kushika nafasi ya nane na ya mwisho kabisa huku akimpiku Laszlo Cseh kwa sekunde .07.
Phelps ana medali 16 za Olimpiki na kushikilia rekodi ya kudumu kwa kutwaa medali nyingi zaidi za dhabahu kuliko mchezaji yeyote akiwa na medali 14, na medali nyingi zaidi kwa michezo binafsi ambapo ameweka kibindoni medai 9.
No comments:
Post a Comment