CHEKA TARATIBU...


Mchana mmoja mtoto alikuwa nje ya nyumba yao akichezea ufagio wa mama yake. Aliendelea na michezo yake hadi alipoitwa ndani na mama yake baada ya giza kuingia. Wakati akiingia ndani akauacha ule ufagio nje nyuma lilipoegeshwa gari. Wakati mama yake akimalizia usafi jikoni akagundua hakukuwa na ufagio pale alipouweka ndipo akamuuliza mtoto ambaye akajibu kuwa uko nje. Mama akasema, "Nenda kaniletee mwanangu!" Mtoto akajibu, "Naogopa mama, nje kuna giza sana." Mama akasema, "Usiogope, kote huko nje yupo Mungu hivyo hakuna cha kukutisha!" Mtoto kusikia hivyo akaenda mlangoni na kufungua kidogo kisha akasema, "Mungu, kama bado uko nje mletee mama ufagio wake!" Duh...

No comments: