WATU 14 WAFA, 50 MAHUTUTI KWA KUPIGWA RISASI UZINDUZI WA FILAMU YA BATMAN...


Nyota wa Filamu ya The Dark Knight Rises, Batman (kushoto)  na Bane (kulia). Katikati ni eneo la tukio baada ya shambulio hilo.
Mtu aliyejificha sura yake amefyatua risasi na kuua wa 14 na kujeruhi wengine 50 wakati wa onyesho la uzinduzi wa filamu mpya ya Batman mjini Denver muda mfupi uliopita.
Mtu huyo mwenye urefu wa futi 6, akiwa amevalia mavazi meusi na kujifunika uso kwa chombo kinachotumika kujikinga na gesi alimimina risasi katika onesho la filamu ya The Dark Knight Rises kwenye jengo moja huko Aurora, Colorado na kuwasha moto ama kulipua bomu la machozi.
Mashuhuda walisema kwamba mtu huyo, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20, aliingia kupitia mlangio wa dharura mbele ya jumba hilo, akiwa kavalia vikinga mwili na na kuanza kumiminia risasi umati kwa kutumia bunduki yake aina ya rifle na bunduki mbili za mkononi huku akipandisha ngazi akishambulia walengwa wake bila mpangilio.
Alisema wanahisi kwamba kuna silaha zaidi zimeachwa kwenye jumba hilo la sinema.
Polisi wamesema mtu mmoja amekamatwa na wataalamu wa kikosi cha mabomu wamepelekwa kwenye jumba hilo, imeripotiwa kwenye taarifa ya habari ya NBC.
Mashuhuda kadhaa wamesema kulikuwa na watoto wao katika uzinduzi huo na mmoja ameripoti kulikuwa na mtoto mdogo katika jumba hilo.
Hospitali kadhaa zimetahadharisha kuwapo ongezeko kubwa la majeruhi na maofisa wa polisi wamekuwa wakifanya kazi ya kupeleka watu hospitali wenyewe, bila kusubiri gari za wagonjwa.
Hayden Miller ameeleza kwamba alikuwa ndani ya jumba la sinema namba 16 na kusikia milio kadhaa ya risasi.
"Kama milipuko midogo ilisikika ikiendelea na muda mfupi baadaye tukasikia watu wakilia kwa maumivu," alieleza.
Hayden alisema mwanzoni alidhani ilikuwa sehemu ya kelele za sinema kutoka jumba linalofuata. Lakini baadaye akaona 'watu wakiinama na kutoka kwenye jumba.'
FBI wamesema wanafanya kazi sambamba na polisi wa kawaida.
Wamesema ni mapema mno kuanza uchunguzi, lakini hakuna uhusiano wowote wa tukio hilo na ugaidi.
Tukio limetokea dakika 30 kabla ya kuanza kuoneshwa filamu hiyo.
Msemaji wa polisi Cassidee Carlson amesema 'eneo la tukio bado lina pilikapilika na tuna taarifa kidogo tutaitoa muda huu."
Msemaji wa Kituo cha Tiba cha Sweden Nicole Williams amesema watu wawili waliojeruhiwa katika onesho hilo wamefikishwa hospitalini hapo kwa matibabu wakiwa katika hali mbaya sana.
Amesema wafanyakazi wa dharura walisema kuna uwezekano wa kupatikana wagonjwa wengine wengi zaidi.
Kwa mujibu wa ripoti ambazo sio rasmi, mfyatuaji risasi huyo alifanya shambulio hilo sababu sinema hiyo mpya ya Batman ilishauzwa.
Aurora iko pembezoni mwa mji wa Denver, takribani maili 10 kusini-mashariki mwa kati ya mji.

No comments: