Utoro wa wabunge uliosababisha Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kushindwa kupita mwishoni mwa wiki kutokana na idadi yao kuwa ndogo, umesababisha Spika Anne Makinda kuweka utaratibu wa kuwalazimisha wabunge kuhudhuria kikao asubuhi na jioni.
Jana wakati akisitisha shughuli za Bunge kwa mapumziko ya mchana, Makinda alisema ameamua wabunge wasaini kitabu cha mahudhurio mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni.
Kabla ya hapo, walikuwa wakisaini mara moja tu asubuhi na kuhesabiwa wamehudhuria kikao cha siku nzima hata wasipohudhuria jioni, lakini sasa itahesabiwa wamehudhuria kikao cha siku baada ya kusaini pia jioni.
Hata hivyo, Spika Makinda hakufafanua sababu za kutaka wasaini mara mbili badala yake alisema:“sababu mnazijua.”
Aidha, wakati akitoa nafasi kwa Mbunge wa Viti Maalumu, Mchungaji Getrude Lwakatare (CCM) kuwa mchangiaji wa kwanza wa Hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Makinda alisema kuna kiashiria kuwa wabunge kweli hawakuwapo bungeni wiki iliyopita.
Alisema hivyo baada ya wabunge kuonesha kulalamika kuwa muda wa mapumziko umefika wakati Lwakatare akizungumza, Makinda aliwakumbusha kuwa muda wa kupumzika mchana umeongezwa kwa robo saa, ambapo badala ya kutoka saa saba kamili mchana sasa watatoka saa saba na robo.
Mbali na kuongezwa robo saa mchana, pia badala ya kikao cha jioni kuanza saa 11 , kitaanza saa 10 kamili ili watoke saa 12 jioni badala ya saa mbili kasoro usiku ili kupisha wabunge waliofunga Ramadhani wafuturu.
Kutokana na mabadiliko hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, jana baadhi ya wabunge walihoji muda kuongezwa, Makinda akasema kitendo hicho kinaonesha hawakuwa bungeni wiki iliyopita.
Hata hivyo, baadhi yao walionesha kutofurahishwa na habari kwamba walitoroka na kusababisha bajeti hiyo kukwama kupitishwa mpaka jana.
Mbunge wa Mkanyageni, Habib Juma Mnyaa (CUF) alisema Bunge si shule, kwamba wanatoroka na kwamba kauli hiyo ya utoro ni ya kuwachafua.
Alifafanua, kwamba wabunge wana shughuli nyingi, zaidi ya kuhudhuria kikao cha Bunge ikiwamo kuhudhuria vikao vya kamati na vingine nje ya Bunge na kwamba wanajua kuwa wamepewa dhamana na wananchi.
Alitoa mfano wa Kamati ya Miundombinu, kwamba jana ilikuwa na kikao na kingeweza kuendelea mpaka wakati wa kuanza kwa kikao cha Bunge na kuhoji kama aliye kwenye kamati anastahili aitwe mtoro.
Kuhusu Jumamosi ambapo kulikuwa na wabunge wachache, chini ya nusu ya idadi yao na hivyo kukwamisha upitishaji wa bajeti, Mnyaa alitoa mfano wa wabunge wa Zanzibar na wengine walioondoka kuwakilisha Bunge kwenye msiba Zanzibar.
Hata hivyo Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali alikiri kuwa baadhi ya wabunge ni watoro sugu, ingawa si wote kwa kuwa wengine huwa na udhuru wa kweli.
Alisema uamuzi wa Spika kuweka utaratibu wa kusaini mara mbili unaweza kupunguza tatizo hilo kidogo, lakini si suluhisho la kudumu.
Alifafanua, kuwa wapo watakaolazimika kusaini jioni na kuona kutokuwapo haja ya kuondoka, lakini pia wapo watakaosaini na kuondoka na wapo watakaokuja mwishoni na kuchukua fomu za kusaini majina muda mfupi kabla ya kusitisha shughuli za Bunge kwa siku husika.
Alipendekeza wabunge warudi katika maadili, wasemane na Spika awe mkali kwa kuongoza kulisimamia hilo ikibidi kuweka hadharani hata majina ya wanaokosekana bila udhuru katika wiki mbili zilizopita. Pia alimtaka Spika kuwa mkali na udhuru ambao umekuwa ukiombwa na wabunge.
Juzi wanaharakati na wasomi waliwakosoa wabunge kwa kukosa kuhudhuria kikao cha Jumamosi iliyopita na kusababisha Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kushindwa kupita na kulazimika Bunge kuahirishwa hadi jana.
Katika hilo wabunge walikemewa kwa kushindwa kuwajibika huku wao wakiongoza kwa kuwajibisha watendaji wa mihimili mingine.

No comments:
Post a Comment