Serikali imesema kiasi cha upatikanaji wa umeme nchini kwa sasa kinakidhi mahitaji, hivyo hakuna suala la nchi kuingia gizani au kuwapo mgawo wa umeme.
Imesema imejizatiti katika hilo, kwani uwezo wa juu wa ufuaji umeme kwa sasa ni megawati 1,375.74 ingawa wastani wa uwezo halisi ni megawati 873 huku wastani wa mahitaji ya nishati hiyo kwa sasa ni kati ya megawati 650 hadi 720.
Akizungumza jana na waandishi wa habari kuhusu taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa mgawo wa umeme unakuja, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi alisema suala hilo halipo.
Aliongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa huduma ya umeme katika kuendesha shughuli za kiuchumi na kijamii nchini, wizara hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ina mikakati ya kuhakikisha unapatikana umeme wa kutosha muda wote bila mgawo.
Maswi alieleza mchanganuo wake wa uzalishaji umeme kuanzia Julai hadi Desemba kuwa mitambo ya nguvu za maji itazalisha kati ya megawati 120 hadi 151 ambayo kwa wastani ni megawati 132 kwa kituo cha Mtera kuzalisha megawati 22, Kidatu megawati 54, Kihansi 60, Nyumba ya Mungu tatu, Hale tatu na Maporomoko ya New Pangani megawati tisa.
Alisema katika mitambo ya gesi asilia kutakuwa wastani wa megawati 348 kwa mchanganuo wa Songas 180, Ubungo 77, Tegeta 41 na Ubungo II (Jacobsen) 50.
Maswi alisisitiza kuwa katika mitambo ya mafuta kutakuwa wa wastani wa megawati 240 ambapo Independent Power Tanzania Limited( IPTL) itazalisha megawati 100, Symbion Dodoma 40, Symbion Arusha 40 na Symbion Ubungo (JetA 1) 60.
Alisema mkakati waliojiwekea ni wa kiwango cha chini sana hadi Desemba ambapo maji huanza kujaa, hivyo hakutakuwa na tatizo hata kama kina cha maji kikipungua kwa kiasi chochote.
Akizungumzia kuiwezesha Tanesco kifedha, Maswi alisema kati ya Agosti mwaka jana na Juni mwaka huu, serikali ilitoa ruzuku ya Sh bilioni 222.4 kwa shirika hilo huku hivi karibuni ikitoa Sh bilioni 25 ili kuhakikisha mafuta ya kutosha yanapatikana ili umeme wa uhakika uwepo.
Alisema ni wazi kuwa Serikali inachukua hatua za makusudi kuhakikisha kunakuwa na umeme wa kutosha na ndiyo maana ikatoa Sh bilioni 247.4 mpaka sasa.
Aliongeza kuwa kwa bahati mbaya kuna baadhi ya wanaodhani kwamba suala la mkopo wa Sh bilioni 408 kwa Tanesco ndiyo njia pekee ya kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika.
Jana baadhi ya magazeti yalidai kuwa hali ya maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme ni mbaya, huku Tanesco ikikabiliwa na ukata mkubwa ambao unaifanya ishindwe kuendesha vyanzo vya umeme wa mafuta na gesi.

No comments:
Post a Comment