SHAMBA LA MICHAEL JACKSON HALIKAMATIKI BEI...

Shamba la Michael Jackson limeongezeka thamani tangu kifo cha mwimbaji huyo, ambapo sasa limezidi thamani ya Dola za Marekani milioni 500 ambazo Mfalme huyo wa Pop aliacha wakati alipofariki.
Nyaraka za kisheria za wasimamizi wa shamba hilo zilizopatikana, zinazoonesha shamba limeendelea kupata thamani zaidi ya Dola za Marekani milioni 475 hadi kufikia mwishoni mwa Mei.
Kwa mujibu wa nyaraka, madeni yote ya Michael Jackson yameshalipwa, isipokuwa tu lile la BIG linalomhusisha uchapishaji wa katalogi ya Michael Jackson, na kwamba wasimamizi watarajia kwamba deni hilo litakuwa limeli lote hadi kufikia mwisho wa mwaka huu.
Sio habari njema kwa shamba pekee, bali pia kwa jeshi dogo la wanasheria waliokuwa wakishughulikia masuala yote ya kisheria na mambo ya kibiashara. Ada yao kuanzia Mei 2010 mpaka Novemba 2011, inazidi Dola za Marekani milioni 13.6!
Vitu vingine viwili ni kwamba, Katherine anataka ziada ya Dola za Marekani 34,700 kwa mwezi kwa ajili ya kuwalipa wanasheria na wahasibu, na Dola za Marekani 205,041 nyingine kwa malipo ya ada ya wanasheria na wahasibu tangu mwaka 2011.
Kitu cha mwisho kabisa ni kwamba kuna madai ya muamana na kesi kadhaa za madai zinazosubiri kutatuliwa.

No comments: