PRODYUZA MKONGWE WA FILAMU ZA JAWS AFARIKI DUNIA...


Richard Zanuck kiwa na mkewe katika moja ya tuzo alizowahi kushinda enzi za uhai wake.
Prodyuza Mkongwe wa filamu za Jaws, Richard Zanuck amefariki kwa ugonjwa wa saratani mapema leo akiwa na umri wa miaka 77.
Alisaidia utengenezaji wa filamu kadhaa kubwa za Hollywood katika kipindi chake cha zaidi ya miaka 70.
Prodyuza huyo mwenye uwezo mkubwa alipata mshituko mkubwa wa moyo nyumbani kwake mjini Beverly Hills asubuhi ya leo.
Alikuwa mtoto wa Mkuu wa Kampuni ya 20th Century Fox, Darryl Zanuck na kuanzia kazi hapo, akifanya kazi upande wa Sauti za Muziki na Ripoti za Chapman.
Lakini baada ya kuwa amefanywa Rais wa kampuni, aliishia kufukuzwa na baba yake kufuatia mfululizo wa makosa ya kizembe, ikiwamo onesho la hovyo kabisa la mwaka 1967 la Dr. Dolittle.

No comments: