MTOTO WALIYEMKATIA TAMAA KUISHI, ASHANGAZA MADAKTARI...

Busu hili laini kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wake limewekezwa na uzito uchungu usioelezeka. Ni kumbatio la mwisho la mzazi; wakati pale Jennifer Lawson aliposema kwaheri ya mwisho kwa binti yake mwenye upendo ambaye aliamini kuwa anakufa.
Madaktari walimweleza Jennifer hakukuwa na matumaini yoyote kwa mtoto wake, Alice aliyekuwa na miezi 14, ambaye alishindwa kuikabili aina ya sumu kali ya uvimbe kwenye ubongo kwa zaidi ya mwezi mmoja kabla. Ugonjwa huo ulisababisha figo kushindwa kufanya kazi, kisha kupooza sehemu kubwa ya mwili. Alice amelala akiwa mahututi kwenye kitanda chake hospitalini, akiwa tegemezi wa mashine ya kusafisha damu kwenye figo na mashine zilizotundikwa za kusaidia upumuaji.
Mashine yake ya kupumulia inakaribia kuzimwa na jopo la wataalamu wa upandikizaji limekaa kando kusubiria miujiza.
Jeniffer ameamua kwamba kutokana na kifo kisicho rasmi cha binti yake baadhi ambayo ni mazuri yatakuja. Viungo vyake vilichangiwa kuwezesha kuokoa maisha ya mtoto mwingine.
Na hivyo anaandaliwa kwa yasiyofikirika; safari ya mwisho kwa binti yake mdogo.
Akiwa kapakata kichwa cha binti yake mikononi, alijisogeza na kugusanisha midomo yake katika uso wa alice, hisia zake zote zilielekezwa kwenye wazo moja: "Nitawezaje kuendelea kuishi bila yeye?"
Leo ameng'ang'ania katika maneno kuelezea maumizu yake.
"Nilikuwa nikijaribu kumweleza jinsi gani tulimpenda; nilitumaini angeweza kunisikia na kuelewa. Niliongea naye kama hakukuwa na tatizo lolote, lakini nilijihisi kupagawa. Haikuwa sawa kabisa. Nilihisi joto lake; nikamwona wa rangi ya waridi mashavuni. Alikuwa akionekana kama mtoto aliyelala.
"Ya kale na yajayo yamekutana kwenye tukio hilo. Nilimweleza ni fahari kiasi gani liyonayo kwake; kwamba kapambana kwa kitambo kirefu na sasa angeweza kupumzika. Na nikajilaza kando yake.
"Nilichanganyikiwa. Walinieleza angefariki asubuhi ile; kwamba walikuwa wakizima mashine sababu asingeweza tena kupumua mwenyewe. Hivyo nilijaribu kujiambia mwenyewe kwamba ameshakwenda, kwamba kilichobaki ni mwili wake mdogo umelala pale. Lakini haikufanikiwa. Unashikilia matumaini ya juu kabisa hadi yanapokwisha kabisa.
"Madaktari walifika kutoa viungo vyake. Mara wakachomoa kila kitu na alikuwa Alice, amelala kitandani kwake huku taa zikimulikia-mulika.
Walimpatia afyuni na kisha tukaacha peke yetu, mimi, Alice na Baba yake, na mshirika wangu Phil.

"Hivyo nilimbusu binti yangu mdogo. Alikuwa na joto sikuweza kuamini alikuwa akikaribia kufa."
Silika ya Jennifer ilikuwa kuthibitisha usahihi. Ambacho kilitokea baadaye ni muujiza.
Alice hakufariki.
Pale mashine yake ya kupumulia ilipozimwa Machi 24, 2010, alianza kupumua mwenyewe, roho yake ndogo haikuondoka.
Si Jennifer mwenye miaka 31, wala Phil Lloyd mwenye miaka 36 ambao waliamini kwamba binti yao wa miezi 14 hakuteleza kutoka kwenye umahututi na kuingia kwenye usingizi wa milele.
"Ukweli haukupambazuka nasi kuanza nao," anakumbuka Phil, "lakini kisha nesi akaja ndani na kusema kitu cha ajabu. Alisema jopo la kuchangia viungo lilikuwa likiondoka; kwamba walikuwa hawahitajiki tena pale. Kisha daktari akaingia na kutuambia Alice alikuwa akipumua bila msaada wa mashine. Walikuwa wakitazama mashine zake kwenye chumba tofauti; waliona kasi yake ya kupumua."
Sasa ni miaka miwili na nusu tangu Alice aliponusa umauti. Leo, akiwa na miaka mitatu na nusu, ni mrembo, mtoto mpenda matoi mwenye macho ya kichina ya bluu, mashavu ya waridi na mwenye tabasamu lisiloisha.
Anaishi na Jennifer, mtaalamu wa zamani wa maseji, Phil, ambaye aliwahi kuendesha duka la urembo kwenye mtandao, na dada yake mkubwa Taylor mwenye miaka nane, kwenye jengo safi Gainsborough, mjini Lincolnshire.
Wote Phil na Jennifer, ambao waliishi pamoja kwa miaka 10, sasa wamejipa majukumu ya kuchangia malezi ya Alice.
Jennifer kamwe hawezi kusahau Siku ya Wapendanao ya mwaka 2010, siku ambayo Alice alianza kuugua.

"Alice alikuwa mtoto mwenye afya, mtoto mwenye furaha, ndio kwanza alianza kupiga hatua zake za kwanza," anakumbuka. "Hakuwahi kuugua zaidi ya maumivu kidogo ya kifua, hivyo sikuwahi kuwa na shaka pale alipoanza kuumwa na kubadilika rangi."

No comments: