Sura yake imevimba, jicho lake la kushoto limevilia damu na midomo yake imetapakaa damu.
Haya yalikuwa majeraha ya kutisha yaliyotokana na adhabu pale Stephanie Hewson alipokabiliana na shambulio la ubakaji.
Shambulio hilo lilikuwa la kutumia nguvu nyingi kiasi kwamba kunusurika kwake na kuendelea kuwa hai ni jambo la kushukuru. Stephanie alikubali kutoa hadharani picha akiamini kwamba picha hizo za kutisha zitasaidia kuwapata waliomshambulia, ambao wamekuwa wakiongezeka katika miaka takribani mitatu.
Polisi pia wametoa picha za kamera za CCTV za mtu wanayemsaka. Stephanie mwenye miaka 26, alishambuliwa baada ya kuwa matembezini usiku akiwa na marafiki zake, akificha utambulisho wake kufafanua majeraha yake.
Alisema: "Ni miujiza kwamba bado niko hai. Nilijeruhiwa kwa kukatwakatwa mgongo wote, juu ya mabega yangu na kichwani, usoni na taya limevimba.
"Macho yangu yalikuwa mekundu na mikwaruzo mwili mzima na niliharibiwa nyuma ya macho yangu yote mawili kufuatia vipigo vya mara kwa mara.
"Pua yangu ilivunjwa na mdomo wangu kuchanwa vipande."
Wakati majeraha yake yanayoonekana kwa macho yanaweza kutibika, Stephanie bado anahangaikia makovu ndani ya kichwa chake.
Alisema: "Tangu lilipotokea shambulio maisha yangu yamegeuka kabisa.
"Sitembei usiku tena, na mara chache mno kutoka kwenda matembezi, kwenye migahawa tu ikiwa ni lazima.
"Nahofia kuteremka kwenye gari kwenda kazini na siendi kabisa matembezini kama ni usiku, hata kama ni supamaketi."
Shambulio hilo lilitokea majira ya Saa 8:33 usiku wa Jumapili ya Agosti 2, 2009 mjini Whitley Bay, Tyne and Wear, ambapo Stephanie alipanga kukutana na marafiki zake baada ya matembezi ya usiku mjini Newcastle.
Alionekana na kundi la watu nje ya Pub ya Envy iliyoko ufukweni mwa mji huo majira ya saa 7:45 usiku kabla ya kuondoka na rafiki yake ambaye waliachana naye saa 8:00 usiku.
Wakati Stephanie mkazi wa North Tyneside akiendelea kutembea, akakutana na mtu ambaye alimkokota nyuma ya kichochoro na kumshambulia kwa lengo la kumbaka.
Polisi walimkuta akiwa amelala kwenye kichochoro, huku akichuruzika damu, baada ya kupewa taarifa na mwananchi mmoja.

No comments:
Post a Comment