MKONGWE ANDY GRIFFITH AZIKWA SAA CHACHE BAADA YA KIFO CHAKE...

Imeelezwa kwamba Andy Griffith ambaye alifariki mapema asubuhi ya jana, ameshazikwa ikiwa ni saa chache baada ya kifo chake.
Mwakilishi wa Kampuni ya Twiford Funeral Homes huko Manteo mjini North Carolina iliyoshughulikia mazishi yake, alisema kuwa Andy alizikwa majira ya Saa 5:30 asubuhi (kwa saa za Marekani) kwenye shamba la familia yake lililoko Kisiwa cha Roanoke.
Imefahamika kuwa hapo kabla andy alitaka kuzikwa mara tu baada ya kifo chake, ndio sababu ikafanyika haraka kiasi hicho.
Juhudi za kutaka kujua kama mwili wa Andy umewekwa dawa ya kuzuia kuoza, lakini hakuna aliyekuwa tayari kuzungumzia hilo ila imeelezwa kwamba ni ruksa huko North Carolina kuzika watu bila kuwekewa dawa za kuzuia miili yao kuoza.
Imefahamika pia kwamba mazishi ya Andy yalifuatiwa na misa fupi iliyofanyika kwa siri na kuhudhuriwa na marafiki wa karibu na familia yake pekee.

No comments: