MAMA APOTEZA WATOTO WAWILI KWENYE AJALI MBAYA, MMOJA AKIWA TUMBONI...

Mama ambaye mtoto wake wa kiume mwenye miaka miwili alifariki kwenye ajali ya gari zilizogongana uso kwa uso amepoteza pia mtoto wake aliyekuwa tumboni, polisi imeeleza jana.
Yeye na mumewe bado wako hospitalini wakiwa katika hali mabaya.
Mwanaume mwenye asili ya Poland, ambaye anaishi mjini Torquay, alikamatwa na polisi kabla ya kupelekwa hospitali ambako baadaye alifariki dunia.
Gari aina ya Vauxhall Vectra alilokuwa akiendesha liligongana na Volkswagen Golf lililobeba familia ya watu watatu mjini Hamelin Way majira ya saa 8:45 mchana.
Polisi jana walikuwa wakichunguza madai kwamba Mpoland huyo alijibamiza kwenye gari la familia hiyo uso kwa uso akikusudia kujiua, kuua mtoto wa miaka miwili na kuwajeruhi vibaya wazazi wake.
Msemaji wa Polisi wa Devon na Cornwall alisema mama mwenye miaka 36 na baba mwenye miaka 39, wanaotokea Ireland, wamefanyiwa upasuaji mbalimbali.
Alisema: "Dereva mwanaume bado yuko chini ya ungalizi makini katika Hospitali ya Derriford, mjini Plymouth na yuko katika hali mbaya akiwa amefanyiwa upasuaji.
"Mwanamke mwenye miaka 36, ambaye alikuwa abiria aliyekaa kiti cha mbele, mwanzoni alipelekwa Hospitali ya Torbay lakini baadaye akahamishwa kwa gari la wagonjwa hadi Hospitali ya Derriford ambako bado yuko katika hali mbaya.
"Mwanamke huyo alikuwa mjamzito na upasuaji ulifanyika kuokoa mtoto aliyekuwa tumboni. Hatahivyo, alifariki dunia."
Barabara ilifungwa kwa zaidi ya saa 10 ambapo magari hayo yalikuwa yakitolewa na upimaji wa chanzo cha ajali ulikuwa ukifanyika.
Timu ya polisi wa kuchunguza uhalifu mkubwa na kitengo cha uchunguzi wa ajali mbaya wote walikuwa wakitafuta kilichosababisha mgongano huo wa magari.
Ajali hiyo ilishuhudiwa na ofisa wa polisi ambaye haraka sana alifika eneo la tukio.
Magari 25 ya huduma za dharura yalifika kwenye ajali hiyo, sambamba na ndege tatu za hudu ya kwanza ikiwamo moja kutoka Dorset, ambayo ilisaidia kuwapeleka waathirika wote wanne wa ajali hospitalini.
Msemaji alisema: "Hali ya hewa wakati huo ilikuwa ya utata, mvua kubwa ilikuwa ikinyesha na kutengeneza mazingira magumu mno ya kufanya kazi kwa huduma za dharura na kuwapa kiwewe wote waliohusika.
"Maofisa Washauri wa Familia wameteuliwa kusaidia familia."
Paul Netherton, Msaidizi wa Mkuu wa Polisi wa Devon na Cornwall alisema: "Hakika hii ilikuwa ajali mbaya sana ambapo huduma za dharura walikuwa wakishughulikia familia eneo la tukio kwenye magari ya wagonjwa na hospitalini, na imekuwa kiwewe kwa wote waliohusika.
"Ulikuwa ajali ya uso kwa uso katika spidi kali. Vectra nyeusi ilikuwa ikishusha mteremko na inaonesha iliserereka na kujibamiza kwenye gari lililokuwa linakuja mbele yake."
Aliongeza mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanaendelea nchi nzima hayakuchangia sababu ya kugongana kwa magari hayo.

1 comment:

Buatbest said...

visit your nice blog~ follow me back~ greeting from MALAYSIA..!!