CHEKA TARATIBU...

Baada ya zaidi ya miaka 30 sasa mwanajeshi mmoja kaona kuna umuhimu wa yeye kutubu makosa yake, hivyo akaenda kwa Padri wake na kusema:
"Tafadhali nisamehe Baba, kwa dhambi niliyotenda. Wakati wa vita ya Kagera nilimficha mateka mmoja darini kwangu."
Padri akajibu, "Sawa! Lakini hiyo sio dhambi."
Mwanajeshi akaendelea, "Lakini nikamfanya akubali kunilipa Dola Ishirini kwa kila wiki anayokaa."
Padri akasema, "Nakiri kwamba haikuwa sahihi, lakini ulifanya hivyo kwa nia njema kabisa."
Mwanajeshi akaruka kwa furaha na kusema, "Ooh, nashukuru sana Padri kwa kunipa amani moyoni mwangu na akilini pia. Nina swali moja la mwisho naomba unisaidie..."
Padri akajibu, "Swali gani tena?"
Mwanajeshi akasema, "Je, sasa ninaweza kwenda kumwambia vita imekwisha?"
Duh, kasheshe...

No comments: