MAMA AKOSA RAHA KUPANGIWA HOTELI ALIMOFIA WHITNEY HOUSTON...

Cissy Houston hakuwa mwenye furaha wikiendi hii pale alipopanga chumba kwenye hoteli ambako binti yake, Whitney Houston alifia...lakini alipata wasaa wa kutembelea chumba alimofia binti yake huyo wakati fulani, imeelezwa.
Mama mzazi wa Whitney yuko mjini Los Angeles wikiendi hii kwa ajili ya Tuzo za BET (ambapo Whitney atatunukiwa) na imeelezwa kwamba alikosa raha pale alipopangishiwa kwenye Hoteli ya Beverly Hilton, hoteli ile ile ambayo Whitney alifariki dunia Februari mwaka huu.
Vyanzo vya habari vimesema Cissy alitaka kutembelea chumba namba 434 kwa kuhitimisha na amepanga kuwasiliana na uongozi wa hoteli hiyo wikiendi hii...lakini kwamba anataka kufanya hivyo kwa wakati wake mwenyewe.
Kwa mujibu wa vyanzo, mapokezi ya Cissy yalihamishiwa Regent Beverly Wilshire badala yake.

No comments: