ALIYEDAI MKE WA USHER RAYMONDS AISHIA WODI YA VICHAA...

Mwanamke aliyekamatwa mbele ya nyumba ya Usher Raymonds wikiendi iliyopita baadaye alipelekwa kwenye wodi ya wenye matatizo ya akili kwa uchunguzi zaidi...baada ya kusisitiza kuwa alikuwa mke halali wa mwimbaji huyo, hii ni kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya kisheria.
Awali ilivujishwa kuwa, Darshelle Jones-Rakestraw alikamatwa nje ya nyumba ya Usher iliyoko Georgia Jumapili iliyopita baada ya kukaidi agizo lililomtaka kukaa mbali na mali za mwimbaji huyo.
Polisi walitoa tahadhari siku moja kabla, pale Darshelle alipoonekana nyumbani kwa Usher kwa mara ya kwanza...na mtu mmoja kwenye nyumba hiyo akalazimika kuita polisi.
Sasa, imepatikana ripoti kutoka polisi ikielezea taarifa zaidi za tukio hilo, ikidai wakati polisi walipowasili Jumapili kufuatia simu iliyopigwa na mtu mmoja, walimkuta Darshelle mbele akiwa anaperuzi kwa kutumia iPad yake.
Kwa mujibu wa ripoti, Usher alimuona mwanamke huyo kwenye kamera yake na kuwaita polisi yeye mwenyewe.
Mara walipomtambua, polisi walimuweka Darshelle chini ya ulinzi kwa kupuuza katazo la kuingia hapo, lakini kwa mujibu wa ripoti alikuwa kwenye hali kama ya wazimu...askari jela walikataa kumpokea.
Kwa mujibu wa nyaraka, Darshelle aliendelea kusisitiza kuwa ni mke wa Usher na kuwa anafahamu yote kuhusu maamuzi yake, jambo ambalo ni maongezi ya kiwendawazimu...sababu Usher bado hajaoa.
Kufuatia hayo, polisi wamedai Darshelle alipelekwa Hospitali ya Emory Johns Creek ambako alipokelewa kwa ajili ya kuchekiwa akili.

Aliachia muda mfupi baadaye...akiwa na nakala ya mashitaka dhidi yake. Darshelle anatarajiwa kufikishwa mahakamani mwezi ujao.

No comments: