KIJANA AUAWA NA CHUI WATATU KWENYE BUSTANI...


Polisi bado wanachunguza kijana huyo aliingiaje kwenye bustani hiyo ya wanyama.
Mtu mmoja ameuawa na chui kwenye Bustani ya Wanyama ya Copenhagen jana baada ya kuruka uzio na kukatiza kwenye handani kuweza kuingia kwenye boma la wanyama hao wawindaji.
Mhanga huyo, ambaye ametambuliwa kuwa na miaka 20 kutoka Afghanistan anayeishi mjini Copenhagen, alishambuliwa na chui watatu baada ya kuruka uzio na kuingia katika bustani ya wanyama iliyoko kwenye mji mkuu wa Denmark mapema asubuhi.
Alikutwa amekufa huku akiwa amezingirwa na chui wakati wafanyakazi wa Bustani hiyo walipowasili kwa ajili ya kazi.
Haijafahamika kwanini mtu huyo aliingia kwenye boma lakini polisi hawakupuuza uwezekano wa tukio la kujiua.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Denmark, kija huyo alikuwa akiishi peke yake kwenye ghorofa lililo jirani na familia yake katikati ya mji wa Copenhagen na alikuwa akikaribia kumaliza masomo yake ya sekondari.
Gazeti la Denmark la Ekstrabladet liliongea na familia ya kijana huyo na ndugu zake mapema jana.
"Tumekuwa tukia siku nzima", mmoja wa wanafamilia alilieleza gazeti hilo.
"Nimekwisha kabisa", mmoja wa rafiki zake alisema.
"Hakika alikuwa mtu mzuri sana."
Mwangalizi wa Bustani hiyo Lars Borg alibainisha kwamba uchunguzi wa mwili wa marehemu umeonesha mtu huyo aling'atwa kwenye paja, kifuani, usoni na kooni.
Alisema: "Tulipokea simu ya dharura majira ya saa 1:30 asubuhi kwamba mtu amekutwa amelala kwenye boma la chui na kwamba chu watatu walikuwa wakirandaranda kumzunguka mtu huyo.
"Chui walimshambulia na kumuua. Inawezekana kabisa kwamba kung'atwa kooni ndio sababu ya kifo chake.
"Alikuwa kwenye maji na wanyama lazima watakuwa walimwona na kumshambulia."
Wapelelezi sasa wanachunguza kupitia picha za kamera ya CCTV kujaribu kujua jinsi mtu huyo alivyoweza kuingia kwenye boma hilo.
Steffen Straede, mtendaji mkuu wa bustani hiyo amesema wataalamu wa saikolojia wameitwa kuzungumza na mfanyakazi aliyegundua mwili huo.
Aliongeza kwamba hili ni tukio la kwanza la aina yake katika historia ya miaka 152 ya bustani hiyo na kwamba hana mpango wa kubadili walinzi.

Alisema: "Kama mtu kweli anataka kuingia pale, hatuwezi kumkinga na kilichotokea."

1 comment:

Anonymous said...

Kijana huyo hajauawa na chui bali na simba milia (tigers)