Mafuriko ya matukio ya kuogofya ya 'mashambulio ya ulaji nyama za binadamu' yameonekana kusambaa nchini China, baada ya dereva wa basi aliyelewa kunaswa na kamera akitafuna uso wa mwanamke katika matukio kadhaa ya kutisha.
Mwanamke huyo asiyekuwa na bahati atalazimika kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa sura bandia kurekebisha uharibifu aliofanyiwa na kichaa huyo aliyemshambulia.
Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo, dereva huyo, aliyetambuliwa kwa jina la Dong, alikuwa akinywa kwa fujo wakati wa chakula cha mchana akiwa na rafiki zake kabla ya kutoka kwa ghafla Jumanne.
Baada ya hapo alikimbilia barabarani katika Jiji la Wenzhou, lililoko kusini-mashariki mwa China, na kusimama mbele ya gari lililokuwa likiendeshwa na mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Du, na kumlazimisha kusimama.
Dong alikwea kwenye boneti la gari hilo na kuanza kugonga gari hilo wakati mwanamke huyo aliyepagawa akipiga mayowe kuomba msaada.
Alipotoka kwenye gari na kujaribu kutoroka, dereva huyo wa basi akamrukia na kuanza kumgalagaza chini.
Hapo ndipo Dong akaanza kumtafuna Du usoni, akimwacha akiwa ametapakaa damu na kulia huku wapita njia wakijaribu kumnasua Dong kutoka kwa mwanamke huyo.
Mashuhuda walisema kwamba dereva wa basi amepata 'kichaa' na kufanikiwa kukabiliana na juhudi za kumpunguza nguvu.
Polisi walipowasili, walifanikiwa kumkamata Dong na kumweka chini ya ulinzi, hivyo kumaliza shambulio hilo.
Du alikimbizwa hospitali, ambako madaktari walisema anatakiwa kufanyiwa ukarabati wa pua na midomo. Tukio hilo ni mfululizo wa matukio kama hayo yaliyofanywa na watu waliochanganyikiwa kutokana na matumizi ya dawa za kulevya nchini Marekani.
Labda tukio lililovuma sana ni lile lililotokea Mei, pale Rudy Eugene alipotafuna uso wa mtu wa mitaani kabla ya kuuawa kwa risasi na polisi.

No comments:
Post a Comment