CHEKA TARATIBU...

Kila mmoja duniani anakufa na kwenda peponi. Mungu anakuja na kusema, "Nataka wanaume wasimame mistari miwili. Mstari mmoja kwa ajili ya wanaume waliowatawala wake zao duniani na mstari mwingine kwa wanaume waliokuwa wakipigwa na wake wake zao. Pia, nataka wanawake wote kuondoka na Mtakatifu Petro."
Alichosema kikafanyika. Kisha Mungu akatazama na kuona wanawake wameondoka na kubaki mistari miwili tu mbele yake. Mstari wa wanaume wanaopigwa na wake zao ulikuwa na urefu wa maili 100, wakati mstari wa wanaume wanaotawala wake zao ulikuwa na mtu mmoja tu.
Mungu akachukia na kusema, "Nyie wanaume lazima muone aibu. Nimewaumba kwa mfano wangu, na wote mmekuwa mkipigwa na wasaidizi wenu. Tazameni huyu mwanangu mmoja aliyesimama na kunifanya nisikie fahari, jifunzeni kutoka kwake!" Akamgeukia yule mmoja na kusema, "Waeleze mwanangu umewezaje kuwa peke yako kwenye huo mstari?
Yule mwanaume akasema, "Sifahamu. Mke wangu ndio kaniambia nisimame hapa."
MWENYEKITI -Mbona sijakiona nyumbani?

No comments: